Manchester City Thread

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
Mechi inayokuja



Matokeo ya Manchester city

 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MAN CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA MWINGINE.​

1640848127929.png

MABINGWA watetezi, Manchester City wamezidi kuwaacha mbali wapinzani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford City usiku wa Jumatano Uwanja wa Brentford Community, Brentford, Middlesex.
Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, Phil Foden dakika ya 16 akimalizia kazi nzuri ya Kevin de Bruyne kumchambua kipa Alvaro Fernandez.
Ushindi huo unaifanya Manchester City imalize mwaka kileleni mwa Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 50, nane zaidi ya mabingwa wa Ulaya, Chelsea wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi 20.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAN CITY YAICHAPA ARSENAL PUNGUFU 2-1 EMIRATES.​


MABINGWA watetezi, Manchester City wametanua uongozi wao hadi pointi 11 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Riyad Mahrez dakika ya 57 kwa penalti baada ya
Granit Xhaka kumchezea rafu Bernardo Silva na Rodri dakika ya 90 na ushei kufuatia Arsenal kutangulia kwa bao la Bukayo Saka dakika ya 31.
Kwa ushindi huo katika mchezo wa 21, Man City inafikisha pointi 53 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 11 zaidi ya Chelsea iliyocheza mechi 29.
Arsenal waliomaliza pungufu baada ya Gabriel kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 59 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Gabriel Jesus wanabaki na pointi zao 35 za mechi 20 katika nafasi ya nne.
1641101244641.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
HALI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA COVID-19 NDANI YA MAN CITY:
◾️
Pep Guardiola na Juanma Lillo wamepata maambukizi.
◾️
Watu 21 ndani ya timu hiyo wamepata maambukizi.
◾️
Wachezaji saba wapo karantini baada ya kupata maambukizi hayo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YASHINDA 4-1 KOMBE LA ENGLAND.​

1641634334099.png
TIMU ya Manchester City imesonga mbele katika michuano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Swindon Town ya Daraja la Tatu usiku huu Uwanja wa The County Ground, Swindon, Wiltshire.
Mabao ya Man City yamefungwa na Bernardo Silva dakika ya 14, Gabriel Jesus dakika ya 28 ambaye pia akikosa penalti dakika ya 62, Ilkay Gundogan dakika ya 59 na Cole Palmer dakika ya 82, wakati la Swindon Town limefungwa na Harry McKirdy dakika ya 78.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAPUNGUZWA KASI ST. MARY'S.​

AVvXsEgJIiCvpGm5xYZ4oY5zb5AEbo9H2tygP0GkQGeqG78_k-c50Phg5Y6dw4OcfFhSLqgcBPW60-2AFmjQcULzx46yQl93Nfl7ugOuALRj838JSNiMWKJ5_deTUe5YpbCDiTYJrve-dE7i-AuYNA8qZlIC9eekDOe7W3Xdarl0lRfp8msZ6y792d98g1EG=s16000

MABINGWA watetezi, Manchester City usiku wa jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's.
Southampton walitangulia kwa bao la Kyle Walker-Peters dakika ya saba, kabla ya Aymeric Laporte kuisawazishia Man City dakika ya 65.
Sare hiyo inaifanya Man City ifikishe pointi 57 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 12 zaidi ya Liverpool wanaofuatia ambao pia wana mechi mbili mkononi, wakati Southampton wanafikisha pointi 25 katika mechi ya 22 na kusogea nafasi ya 12.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAHREZ APOZA MACHUNGU YA AFCON MAN CITY.​

AVvXsEggomLxqcJnvXte9kko-q6silwgfj1KAKHUjrkCC-GsYSPPyChXtDtcfvPnPruQGAzdwl45ZldHeHT5dkz48AUY_qdzz-34bXAP10a5tT5dn7pAek3CaQGPsVPJtSWUvvs8HbXlX--uqgvCbJzfZ0oVgZWoDpNPwaZQJ2BFYxTS0A8wIM45ZLv8O5mP=w640-h428

MSHAMBULIAJI Riyad Mahrez jana aliweka kando machungu ya kushindwa kuisaidia Algeria kutetea taji la AFCON baada ya kufunga mabao mawili kuiwezesha Manchester City kuichapa Fulham 4-1 usiku wa Jumamosi Uwanja wa Etihad na kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la FA England.
Mahrez alifunga dakika ya 53 kwa penalti na 57, wakati mabao mengine ya Man City yalifungwa na İlkay Gündoğan dakika ya sita na John Stones dakika ya 13, wakati bao pekee la Fulham lilifungwa na Fabio Carvalho dakika ya nne.
Nayo Chelsea ililazimika kusubiri hadi dakika 120 kusonga mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Plymouth Argyle Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Beki, Macaulay Gillesphey alianza kuifungia Plymouth Argyle dakika ya nane kabla y The Blues kutoka nyuma kwa mabao ya César Azpilicueta dakika ya 41 na Marcos Alonso dakika ya 105 na ushei.
Naye Harry Kane jana alifunga mabao yote, Tottenham ikiichapa Brighton 3-1 na kutinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA England. Bao pekee la Brighton lilifungwa na Yves Bissouma.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAHREZ AFUNGA MAN CITY YASHINDA 2-0.​

AVvXsEh-UCLNTnG2YOuqOgFCNskGDTkNLm3pN9I03Sl-ZCZ7X8b1543iNQ9PssjbltIzCU2qtmZbzAk9bLlYu7Ik3mEgv6f9r17QV6Knx4xFOx0aX4_MGtCfBvWEt3BcOyTyeJFx2iPTn_lRFXKxP_S3im7BX5RZ4qLs8xdMyoapC5E5DtaOEqdQhslXOvFN=w640-h426

WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad.
Mabao ya Man City yamefungwa na Mualgeria Riyad Mahrez dakika ya 40 kwa penalti baada ya Raheem Sterling kuchezewa rafu na Mads Roerslev wa Brentford na la pili, Mbelgiji Kevin de Bruyne dakika ya 69 akinufaika na makosa ya David Raya.
Sasa kikosi cha kocha Mspaniola, Pep Guardiola, Manchester City kinafikisha pointi 60 katika mchezo wa 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 12 zaidi ya Liverpool inayofuatia ambayo pia ina mechi mbili mkononi, wakati Brentford inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 sasa katika nafasi ya 14.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

STERLING APIGA HAT TRICK MAN CITY YAUA 4-0.​

AVvXsEhZYAQHmkLUDHNHmN80slxt8Tlxgg6joiXZlnD42eJty_0XVHowDcefgEHkvrpAw6L87W33P_FnqusQexGVMtidYqFOdpiV7meUEi5BwL5DxIhrkZt69lHzWYkeyYHf4bjeLcuXS807_NtOFM8XhU8YvH5Tj-t-I9EH3-18J09xLo5rMlJynNytjYvY=w640-h426

TIMU ya Manchester City imeibuka na ushindi wa 4-0 ugenini dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Carrow Road,
Mabao ya Man City yalifungwa Raheem Sterling aliyepiga hat trick kwa mabao yake ya dakika za 31, 70 na 90 huku bao lingine la Man City likifungwa na Philip Foden dakika ya 48.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
🗣️
Guardiola kuhusu Bernardo Silva:
"Anaweza kucheza na kufanya majukumu zaidi ya sita uwanjani, hachezi tu mpira, anauelewa mpira"
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na maandishi yanayosema 'MAN CITY 2 CIT'
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAN CITY YAIFUMUA UNITED 4-1​


WENYEJI, Manchester City wamewafumua jirani zao, Manchester United mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne mawili dakika ya tano na 28 na Riyad Mahrez mawili pia, dakika ya 68 na 90, wakati la Man United limefungwa na Jadon Sancho dakika ya 22.
Kwa ushindi huo mnono, timu ya kocha Mspaniola, Pep Guardiola inafikisha pointi 69 katika mchezo wa 28 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi sita zaidi ya Liverpool wanaofuatia, ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
Kipigo cha leo kinazidi kupunguza matumaini ya Man United iliyo chini ya kocha wa muda, Mjerumani, Ralf Rangnick kumaliza nafasi nne za juu, ili ikibaki na pointi zake 47 za mechi 28 nafasi ya tano.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAIFUATA LIVERPOOL KIBABE WEMBLEY​

E3D21AB3-1163-42DA-90DA-744BBD09EA53.jpeg

TIMU ya Manchester City imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England kwa kishindo baada ya kuwachapa wenyeji,Southampton mabao 4-1 Jumapili Uwanja wa St. Mary's mjini Southampton, Hampshire.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 12, Kevin De Bruyne dakika ya 62 kwa penalti, Phil Foden dakika ya 75 na Riyad Mahrez dakika ya 78, wakati la Southampton limefungwa na Aymeric Laporte aliyejifunga dakika ya 45 na ushei.
Sasa Man City itakutana na wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool mwezi ujao Uwanja wa Wembley Jijini London.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAN CITY YAWACHAPA BURNLEY 2-0 TURF MOOR​


MABINGWA watetezi, Manchester City jana walipata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin de Bruyne dakika ya tano na Ilkay Gundogan dakika ya 25 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi
73 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool, baada y wote kucheza mechi 30.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY NA LIVERPOOL SARE 2-2 ETIHAD​


WENYEJI, Manchester City wamelazimishwa sare ya 2-2 na wapinzani wakuu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Kevin De Bruyne alianza kuwafungia City dakika ya tano tu akimalizia pasi ya Bernardo Silva, lakini Diogo Jota akaisawazishia Liverpool dakika ya 13 akimalizia pasi ya Trent Alexander-Arnold.
Gabriel Jesus akaitanguliza tena Man City dakika ya 36 akimalizia pasi ya João Cancelo, kabla ya Sadio Mané kuisawazishia Liverpool dakika ya 46 akimalizia pasi ya Mohamed Salah.
Kwa sare hiyo, Manchester City inafikisha pointi 74 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 31.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YASHINDA 3-0, YAREJEA KILELENI​


MABINGWA watetezi, Manchester City wameibamiza Brighton & Hove Albion mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Riyad Mahrez dakika ya 53, Phil Foden dakika ya 65 nw Bernardo Silva dakika ya 82.
Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 77 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 32 na Brighton inabaki na pointi zake 40 za mechi 33 nafasi ya 10.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MAN CITY YAITANDIKA NEWCASTLE UNITED 5-0 ETIHAD​



WENYEJI, Manchester City wamepiga hatua moja mbele kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Newcastle United leo Uwanja wa Etihad, Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Raheem Sterling mawili, dakika ya 19 na 90 na ushei, Aymeric Laporte dakika ya 38, Rodri dakika ya 61 na Philip Foden dakika ya 90 na kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 86 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 35.
Newcastle United wao wanabaki na pointi zao 43 za mechi 36 sasa nafasi ya 13.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

DE BRUYNE APIGA NNE MAN CITY YAICHAPA WOLVES 5-1​


MABINGWA watetezi, Manchester City wameitandika Wolverhampton Wanderers mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Molineux, Wolverhampton, West Midlands.
Nyota Mbelgiji, Kevin De Bruyne peke yake amefunga mabao manne dakika za saba. 16, 24 na 60, kabla ya Raheem Sterling kufunga la tano dakika ya 84, wakati la Wolves limefungwa na Leander Dendoncker dakika ya 11.
Man City imefikisha pointi 89, tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 36.
Wolves wanabaki na pointi zao 50 za mechi 36 pia nafasi ya nane.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY YAAMBULIA SARE KWA WEST HAM, 2-2 LONDON​


MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa London Jijini London.
West Ham walitangulia kwa mabao ya Jarrod Bowen dakika ya 24 na 45, kabla ya Man City kuchomoa kupitia kwa Jack Grealish dakika ya 49 na Vladimír Coufal aliyejifunga dakika ya 69.
Manchester City ingeweza kuondoka na pointi zote tatu kama mshambuliaji Mualgeria, Riyad Mahrez angefunga penalti dakika ya 86, ambayo iliokolewa na Fabianski. Penalti hiyo ilifuatia Gabriel Jesus kuangushwa na Craig Dawson kwenye boksi.
Man City inafikisha pointi 90 katika mchezo wa 37 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi, wakati West Ham sasa ina pointi 56 za mechi 37 nafasi ya saba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAN CITY BINGWA TENA ENGLAND, LIVERPOOL...​


TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa mwisho leo Uwanja wa Emirates Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 76 na 81 na Rodri dakika ya 78 baada ya Villa kutangulia na mabao ya Matty Cash dakika ya 47 na Philippe Coutinho dakika ya 69.
Manchester City inamaliza na pointi 93, ikiizidi pointi moja Liverpool baada ya mechi 38 za msimu.
Liverpool imemaliza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Anfield katika nafasi ya pili.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 24, Mohamed Salah dakika ya 84 na Andrew Robertson dakika ya 89, baada ya baada ya Pedro Neto kuanza kuifungia Wolves dakika ya tatu.
Chelsea imemaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na kufikisha pointi 74 mbele ya Tottenham Hotspur ya nne iliyomaliza na pointi 71 baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Norwich City.
Arsenal imemaliza nafasi ya tano baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Emirates na kufikisha pointi 69.
Manchester United imemaliza nafasi ya sita licha ya kuchapwa 1-0 na Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park Jijini London ikibaki na pointi zake 58.
Burnley iliyomaliza na pointi 35, ikizidiwa tatu tu na Leeds United, imeungana na Watford na Norwich City kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu.
Mohamed Salah wa Liverpool ndiye mfungaji Bora kwa mabao yake 22, mbele ya Son Heung-Min wa Tottenham aliyemaliza na mabao 21 na Cristiano Ronaldo wa Man Utd mabao 18.