Manchester City wakutwa na Mashtaka ya kujibu.

Feb 7, 2023
61
36
5
Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza imekumbwa na mashtaka mbalimbali baada ya Uchaguzi uliofanywa na bodi ya ligi kuu Uingereza.
Mashtaka hayo wanayokabiliana nayo ni zaidi ya 100 kuanzia 2009 mpaka 2018 ambapo katika kipindi hiki cha miaka 9 Man city walitwaa mataji 3 ya ligi kuu.
Baadhi ya mashtaka wanayokabiliana nayo miamba hiyo ya Manchester ni pamoja na;
-Kushindwa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi (2018/19 2022/23)
—Kuzidisha mapato ya wadhamini na kuficha ukweli wa vyanzo vya mapato
—Kumlipa kocha Roberto Mancini pesa zaidi kwenye mkataba wa siri
—Kushindwa kutoa taarifa halisi kuhusu mishahara ya wachezaji
—Kuvunja sheria za faida na uendelevu za Ligi Kuu England
—Kushindwa kuendana na taratibu za mapato na matumizi ya UEFA
Kama Manchester City watakutwa na makosa haya basi wanaweza kukumbana na adhabu ya kushushwa daraja, kulipa faini, kutoshiriki michuano ya UEFA.
Hata hivyo Manchester City wenyewe wamekana kuhusika na mashtaka hayo, hivyo wapo tayari kupelekea kesi hiyo mahakamani.
Je,unaiona wapi Manchester City katika kesi hii inayowakabili wana nafasi ya kushinda au watakumbana na adhabu?
 

Attachments

  • 20230208_082039.jpg
    20230208_082039.jpg
    390 KB · Somwa: 0
  • Like
Reactions: Bangala