
Baada ya kuwa nje kwa muda ni rasmi sasa kipa namba Moja wa klabu ya SIMBA, Aishi Manula ameanza mazoezi mepesi ya kuurudisha utimamu wake wa mwili katika Uwanja wa MO SIMBA ARENA uliopo BUNJU
Manula alifanyiwa matibabu Afrika Kusini baada ya kuumia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Aprili 7 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Una Mategemeo Yapi Kutoka Kwake?