MAONI YA DR. PALLANGYO KUHUSU SAKATA LA FEISALI

Nabi

Mgeni
Nov 4, 2022
121
124
5
Hapo awali nilichagua kutoongea kabisa kuhusu suala Hili la Feisal kutokana na sababu kadhaa na niliamini litapita na kwa sawa kutokana na kwamba nilikuwa nimeongea naye Mara kadhaa

Nina Machache nataka nimkumbushe Feisal na kuwafahamisha wanamichezo wote

1, Yanga sc Tarehe 12 jul 2018 saa 7:27 mchana maeneo ya Temeke yalimalizika mazungumzo na makubaliano ya pande zote tatu Yanga sc, Singida United na Feisal mwenyewe Rasmi akawa mchezaji wa Yanga sc

Alisaini mkataba wa kuitumikia Yanga sc kwa mkataba wa miaka miwili na mshahara wa Tsh 1.6 million alitumikia mkataba wake Hadi ulipomalizika na mwaka 2019 mwishoni mkataba wake ukiwa mwishoni aliongeza mkataba mwingine wa miaka minne wenye kipengele Cha kuongeza mshahara kutoka 1.6 milion Hadi lufikia Tsh milion 4 na bonasi kadhaa

Alianza kuutumikia rasmi mkataba wake 2020 mwanzoni na mwishoni mwa mwaka 2020 ufadhili Wa GSM ulitua mitaa ya jangwani Rasmi walifanya sajili kadhaa za akina Yikpe, sadney Ukrhob kindoki na wengineo usajili haukuzaa matunda na hakuna na Ni sadney Ukrhob aliyekuwa akimzidi Feisal mshahara alikuwa akipokea Tsh 4.7 milion kwa mwezi 2021 Yanga sc ikawaondoa wengi na kuleta wengi akiwemo mukoko Tonombe na Tuisila kisinda usajili haukuzaa matunda pia

Mwaka 2022 waliletwa wengine wakiwemo Djuma shabani, bangala, Mayele na wengineo hatimaye usajili ukazaa matunda na kupeleka kombe jangwani nyakati zote ambazo Yanga sc walifeli walikuwa wakiongeza wachezaji wenye Profile kubwa na wenye majina makubwa hivyo na mishahara yao ilikuwa mikubwa pia

Mwaka huu Yanga sc wameongeza wachezaji wengine wenye Profile kubwa zaidi kwa kuwaleta akina Aziz KI Musonda na kumrudisha morison ni wakati huu ndipo Feisal akaibuka na kuongea maneno kadhaa yanayoonyesha yeye anaonewa

Nichukue nafasi hii kumkumbusha Feisal kipindi amesaini Yanga sc alikuwa ndiye mchezaji anayepokea mshahara mkubwa zaidi Yanga sc na mama yake aliyeongea na vyombo vya habari Leo hii Ni shahidi wa hili pia nimkumbushe Feisal na watu wake kwamba ameitwa ofisini Mara 5 kwa ajili ya kujadili suala la yeye kusaini mkataba mpya

Nimkumbushe Mara ya mwisho kwenda pale jengo la GSM malls Posta mwezi November ilikuwa siku ya Ijumaa baada ya swala ya mchana makubaliano ya mwisho yalikuwa atasaini mkataba mpya wenye mshahara wa Tsh million 14.6 na bonasi binafsi

Je kwenye Hili ubaya wa Yanga sc unaohubiriwa na watu kadhaa wakiwemo mapunguani na mazuzu kadhaa ya E FM Wakiongozwa na Jemedar Said na Wilson Oruma Ni upi au mnataka kujibiwa ili mpate umaarufu zaidi

Mnadhani mnamuharibia Nani Yanga sc au Feisal??? Baada ya kuangalia video ya mama yake na Feisal nimerudi kutafakari upya juu ya kutenda wema kwa watu wasio wema wakati ukidhani Ni wema Kuna mengi Sana sijaandika hapa juu ya Feisal na Yanga sc

Dr. Furahini isack Pallangyo