MASHABIKI WAMTAJA ALABA KAMA YUDA

McRay

Mgeni
Nov 4, 2022
185
131
5
MASHABIKI WAMTAJA ALABA KAMA YUDA.

Mashabiki wa Klabu ya Real Madrid wameanzisha kampeni ya Klabu yao kumwondoa Klabuni Mchezaji wao,David Alaba kufuatia Kumpigia Kura Lionel Messi kama Mchezaji Bora namba Moja wa Dunia huku Mchezaji mwenzake wa Real Madrid,Karim Benzema akimweka nafasi ya pili na ya tatu akiwa ni Kylian Mbappe.

Mashabiki hao wanamuona Alaba ambaye amepiga Kura kama Nahodha wa Timu ya Taifa ya Australia amemsaliti Mchezaji mwenzake,Karim Benzema ambapo wanaamini alistahili zaidi ya Messi.

Kupitia account za Twitter Mashabiki hao wamekuwa wakindika #AlabaOut na hata kwenye Post zake za Instagram wamekuwa waki-comment kwenye comments Kwa kuandika #AlabaOut

Mwaka 2013 Alaba aliwahi kuonesha Mapenzi yake ya wazi wazi Kwa Lionel Messi ambapo alipost Caption iliyokuwa inaashiria furaha Baada ya Messi kufunga goli.

0C72C211-82A9-4A33-A8CD-D9FEFC8A3D79.jpeg