Mashabiki wetu wanahitaji zaidi hamasa kujaza uwanja

Feb 7, 2023
61
36
5
Kuelekea michezo ya kimataifa Wikiendi hii,Simba na Yanga watakuwa uwanja wa Mkapa kuwakaribisha wapinzani wao.

Simba wataanza siku ya jumamosi kuwakaribisha Raja Casablanca wakati Yanga watawakaribisha Tp Mazembe.

Ili kufanikiwa kupata hamasa ya mchezaji wa 12 ambae ni shabiki, ni lazima apewe hamasa kubwa ya kuja uwanjani lakini pia kupunguza bei za viingilio.

Simba kuwahamasisha mashabiki wao kujaza uwanja ili kuwa kawaida yao,walikuja na kampeni ya "Kispika mtaa kwa mtaa" na walifanikiwa kwa asilimia kubwa kushawishi mashabiki.

Yanga wao walikuwa na njia nyingine kabisa ambayo unaweza kusema kwa asilimia kubwa haikufanikiwa,hivyo kuamua kufanya kama wapinzani wao kuwafuata mashabiki mitaani.

Hamasa ya mashabiki kama mchezaji wa 12 uwanjani inawapa wachezaji nguvu na ari ya kupambana zaidi kwa matokeo ya ushindi.

Hivyo kila la kheri Simba na Yanga, naamini Benjamin Mkapa Jumamosi na Jumapili utakuwa FULL HOUSE mashabiki 60,000.20230216_095010.jpg