Mchawi wa Simba Ni Simba wenyewe

Stuart 04

Mgeni
May 3, 2024
17
4
5
Mimi nilikuwa nadhani baada ya mzunguuko wa kwanza kukamilika Simba walishaona wapi wamekose, sijategemea Kama wangeingia kwenye presha za usajili tena
vipi Kama wangeatulia kuanzia dirisha dogo wangesajili key players wa maana kwa malengo ya msimu ujao..? Namaanisha mzunguuko wa pili ungekuwa kwenye malengo ya kutengeneza naamini msimu ujao Simba wangekuwa wa Moto saana
Tuangalie ile yanga ya NABI alipoanza nayo ampaka anakuja kubeba ligi alikuwa kwenye kutengeneza timu na aliichukua timu mzunguuko wa pili wakati upo mwanzoni mwanzoni na msimu uliofuata alimaliza kwa kubeba kombe la ligi, why Simba.
Sidhani Kama wanatakiwa kumtafuta mchawi wa hii Vita ya better performance ikiwa hawataki kukubaliana na uhalisia wa timu inavyotaka na sitegemei Kama msimu ujao Simba atabeba tena kwani ataenda kuacha rundo la wachezaji na kuhitaji wachezaji wengi kuongeza ili kutengeneza timu maswali ya kizushi SASA JE ATAWEZA KUWAUNGANISHA WACHEZAJI WOTE KWA KUTUMIA PRE SEASON TUU..? JE ATAWEZA KUWAPATA WACHEZAJI WOTE BORA ANAOWAHITAJI..?
N.B anapotumia kipindi Cha usajili lazima ajue Ni wakati wa kila timu kujiuliza kwahiyo kila mtu yupo sokoni anachotakiwa Simba Ni kuhakikisha hawakosi Target

NAWASILISHA STUART_04