Mchezaji anaelipwa Hela nyingi Kumzidi Ronaldo.!

kidudumtujr

Mgeni
Dec 14, 2022
50
70
5
Tanzania
Watu wengi wanajua Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji tajiri zaidi baada ya kulamba dili la usajili mnono kuliko mchezaji yoyote kwa sasa.

Ronaldo ana utajiri wa paundi milioni 425 ambazo anazipata kutokana na mikataba ya makampuni mbalimbali kama vile Armani, Uniliver, Nike, Herbalife na Dazn.

Madili yote haya yanamuingizia Ronaldo kiasi cha paundi milioni 34 kwa mwaka.

Alikuwa anaingiza paundi milioni 62.5 kwa mwaka alipokuwa anaichezea Manchester United.


Lakini baada ya kujiunga na klabu ya Al- Nassr ya Saudi Arabia, Ronaldo anaingia paundi milioni 173 kwa mwaka .

Na kama atakaa miaka 7 klabuni hapo kama mkataba wake unavyosema, basi atajiingizia kitita cha paundi bilioni 1.3.

Hii inamfanya Ronaldo awe ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa kuliko wote.

Lakini licha ya kipato chote alichonacho, Ronaldo anazidiwa utajiri mara 15 na kijana mdogo tu.

Si mwingine bali ni Faiq Bolkiah, mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya Arsenal.

Kijana huyo ana utajiri wa paundi bilioni 20.

Licha ya ukweli kuwa hajulikani sana katika ulimwengu wa soka, lakini ndiye mchezaji tajiri kwa sasa kuliko wote .

Bolkiah, mwenye miaka 23, amezaliwa katika familia ya kitajiri yenye kujihusisha na biashara ya mafuta.

Baba yake ndiye sultani wa kisiwa cha Brunei.

Hata hivyo, licha ya familia yake kujihusisha zaidi na biashara ya mafuta, mapenzi yake yapo katika mpira wa miguu.

Alianza kucheza mpira akiwa mdogo nchini Uingereza katika vilabu vya Southampton, Chelsea, Reading na Arsenal.

Baadae alijiunga na klabu ya Leicester mwaka 2016 ikiwa ndio mara yake ya kwanza kucheza kama mchezaji wa kulipwa.

Sasa hivi anaichezea timu ya Chonburi ya Thailand akitokea klabu ya Maritimo Desemba 2021.4AE77619-1E19-4BD7-BDBE-B8D4C1C966AF.jpeg