Mechi Dume

Feb 7, 2023
61
36
5
Barcelona walianza vizuri sana kabla ya pedri kuumia kipindi cha kwanza,kivipi?

Kwenye karatasi wameningia na 4-3-3,lakini wakati wanafanya build up nyuma wanabaki mabeki watatu(Kounde,Araujo na Alonso) wakati mbele yao kuna kuwa na Kessie na DeJong mbele tena kuna namba kumi wawili Pedri na Gavi ambaye anatoka pembeni na kuingia ndani wakati mstari wa mbele Alaba, Lewandowski na Raphina hivyo wanatengeneza 3-2-2-3.

Silaha yao kubwa ilikuwa upande wa kushoto ambapo Alaba alikuwa anafanya Overlapping sana, hii inatoka na Gavi kumvuta Bissaka ndani hivyo kuacha nafasi kubwa iliyokuwa inatumiwa na Alaba,walichoshindwa ni kuweka mpira wavuni.

Manchester wao waliingia na 4-2-3-1,lakini walifanya zaidi high pressing kwa kutumia 4-1-4-1 Casemiro akibaki kwenye namba sita peke yake juu yake Sancho,Bruno,Fred na Rashford huku juu yao Weghorst.

Baada ya Barcelona kupata goli,United waliamua kufunguka na kuleta madhara kwenye eneo la Barcelona ambao wao waliamua zaidi kukabia juu na kuacha nafasi nyuma yao ambayo ilikuwa inatumiwa na Rashford,Sancho.

Timu zilipishana zaidi kipindi cha pili

De gea anastahili kupongezwa kwa saves alizofanya leo.

Rashford kafunga goli lake la 22 kwenye michuano yote mpaka sasa.

Mbungi inaenda kumaliziwa OT

20230216_234123.jpg
 
  • Like
Reactions: sharon