MEXICAN WAVE

Capitano

Mgeni
Nov 8, 2022
10
29
5
Mexican Wave


Hii ni aina ya ushangiliaji ambapo mashabiki uwanjani hushangilia kwa style moja, na pindi inapotokea Mexican wave uwanjani wakati wa mechi, hii inadhihirisha kuwa watazamaji wanafurahia mchezo.

Namna ya kushangilia ni kuinuka na kuinua mikono juu kwa awamu kuzunguka uwanja mzima.

Asili ya mtindo huu wa ushangiliaji (Mexican wave) ilianzia kwenye mchezo wa American football nchini marekani kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1980, lakini ushangiliaji huu ulipata umaarufu kimataifa miaka michache baadae kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini Mexico mnamo mwaka 1986 na ndipo ulipewa jina hilo la Mexican Wave.

Na ushangiliaji huu mara nyingi huonekana kwenye mashindano ya kombe la dunia, mfano kwenye World Cup hii tumeona kwenye mechi kama ya Portugal dhidi ya Switzerland, Spain dhidi ya Costa Rica, bila shaka na mechi nyingine imefanyika hii Mexican wave.

Tuendelee kutazama, kufurahia na kufuatilia mashindano haya ya kombe la dunia kutoka nchini Qatar, bila shaka tutaona ushangiliaji huu wa kuvutia sana wa (Mexican Wave) ukitokea viwanjani.
 
  • Like
Reactions: McRay and Nabi