Mjadala kwamba Morocco sio Afrika ni mjadala wa kibaguzi

Zawadi

Mgeni
Nov 4, 2022
41
17
5
Mjadala kwamba Morocco sio Afrika ni mjadala wa kibaguzi. Aficanism is not a race it's Ethinicity. Ndio maana Kanye West ni mweusi kama Muha wa Kazuramimba lakini hataki kuitwa Mwafrika. Anaajiita black America. Malabuku 🤣.

Being an African means where u belong to, not your race. Uwe mweusi, mweupe, wa manjano, au orange kama mabehewa ya TRC wewe ni mwafrika tu. Ndio maana Wasomali ni waafrika wenzetu japo sio weusi kama Wamanyema. Comorro ni waafrika wenzetu japo hawana hips kama Wasonjo. Kufikiri kwamba ili uwe Mwafrika lazima uwe na ngozi nyeusi kama Mjaluo ni mawazo kindugai 🤣.

Morocco are Arabs by race but Africans by Ethinicity. Morocco imeshiriki harakati za ukombozi wa Africa Sub Sahara. Mfalme Hassan II ni miongoni mwa Waasisi wa OAU japo baadae alijitoa kufuatia mgogoro wa Western Sahara. Morocco tunacheza nao mashindano mbalimbali ya soka Afrika kama wafrika wenzetu. Hata nafasi ya kwenda World cup wameipata kupitia Africa lakini leo tunawakataa. Ilikuaje tukawapa watu wasio waafrika nafasi ya kuwakilisha Afrika kwenye kombe la dunia? Futuhi. Ndio ni Futuhii 🤣.

Tukiwabagua Morroco kwa rangi yao, kesho tutasema Wapemba sio Waafrika maana rangi yao sio kama Wafipa. Tutasema Madagascar sio Afrika kwa sababu asili yao ni Tiger Asia, au Sychelles sio Afrika maana asili yao ni Ufaransa, na tutasema Wachagga sio waafrika maana asili yao ni Israel (kidding 🤣).

Anyway, kwa kifupi ukizaliwa kwenye hili bara wewe ni Mwafrika utake usitake (kwa sauti ya Ndugai). Labda uamue kujibagua mwenyewe na kujiona sio mwafrika. Hatuwezi kung'ang'aniza undugu na mtoto wa George Weah aliyezaliwa na kukulia Marekani kwa sababu tu ni mweusi, lakini Wamorocco waliozaliwa kwenye ardhi ya Afrika tunaona si wenzetu kwa sababu ni weupe. Upuuzi.!

Yani timu za Morocco tucheze nazo klabu bingwa Afrika, kombe la shirikisho na kombe la mataifa ya Afrika bila kuona Uarabu wao, lakini inapofika kombe la dunia eti ndo tuwaone Waarabu? Huo ni unaa (kwa sauti ya Lyatonga Mrema 🤣). Tunaoamini Morocco ni Afrika acha tufurahie ushindi. Nyie mnaoamini sio Afrika subirini Burundi icheze World cup ndo mshangilie. Tusichoshane.! 🤣
 
Last edited:
  • Like
Reactions: sharon