Mmeshinda lakini mna furaha?? Yanga Pointi 7 nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi

Bangala

Mgeni
Dec 13, 2022
39
24
5
Leo Yanga mmejitahidi ila inabidi wawe wanaandaa wapiga penalt wazuri na sio mtu yeyote tuu au kubahatisha. Mayele ajifunze umakini akifika golini na kutaka kufunga na asitake afunge yeye tuu hata kama hana nafasi nzuri ajifunze kutoa pasi kwa wenzake.

Yanga tunashida mbili endelevu.. mipira ya set pieces na wapigaji wa penalty nadhani hatuna mazoez ya kutosha.

Fantastic display.... Mudathir ni aina ya mchezaji anayehitaji muda wa kufikiria akiwa na mpira, he has to be quick, lasivo watakuwa wanampress wanamnyang'anya kama leo

Mayele akiwa anakimbia kuelekea goli usitegemee atakupasia sometimes anapoteza clear chances.

Tunahitaji winga mmoja wa kisasa anaeweza kukimbia kuelekea ndani, in modern football ukikimbilia pembeni wanakuacha wanakaba alie kwenye box ukipiga tu cross inapotea

Pia Timu leo haikuwa organized sawa sawa Tumepoteza nafasi ikiwemo Penalt na wachezaji kunyimana pasi muhimu kwaajili ya kufunga goli. AzizKi ,TuisilaKisinda ,Bangala ,Musonda wote hawakuwa mchezoni leo.

1678340587477.png
 

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
Big point mudathir leo kama hakuwa mchezoni mpira unaowewe na unanyang'anywa kweli, azizi ki Nae sijui ni Presha ya mchezo.....kunawakati wamechezewa kama wao ndio wagen....mmh
 

Clara

Mgeni
Dec 13, 2022
20
6
5
Waarabu kuna wakati wanaonekana bora kwasababu ya umakini wao kwenye nafasi wanazopata wanazitumia vizuri,hii mechi ilikuwa ya kushinda hata goal 5 kama umakini ungelikuwepo.bado kuna tatizo kwenye umaliziagi.
 

JohBwax

Mgeni
Nov 4, 2022
84
72
5
Note the name Ibrahim Sidibe na Mousa koulibaly hao jamaa timu imefungwa lakini wao wameondoka mashujaa, jamaa wamekichafua sana
 

Nabi

Mgeni
Nov 4, 2022
121
124
5
mimi naliona ili ama, timu zetu zimekosa uwezo wakupiga pasi zikafika kwa mlengwa ni wachezaji wachache wanaofikisha pasi mipira mingi inapotea kwenye kupasia tatizo ni nini ? Juzi niliona Simba wakistragol kwenye kupasiana jana tena nimeona Yanga nao tatizo ni lile lile, sasa sijui makocha hilo tatizo wameliona! Na kama wanataka kufanya vizur huko wanakotaka kwenda warekebishe ilo tatizo vinginevyo wakikutana timu yenye ukatili mbele ya lango wataadhibiwa mnoo