Mo Dewji Tafuta STRAIKA Wa Maana Umalize Kazi Uliyoianza

May 27, 2024
7
2
5
Leo sitasema sana maana yanayotakiwa kusemwa nimeshayasema kwa siku kadhaa sasa zilizopita.

Baada ya hongera nitaongeza neno moja tu kwa Mwekezaji Mo Dewji. Baada ya usajili mzuri ambao kiukweli unaridhisha sana na kabisa unaona watu wa maana wanaojua mpira walikaa chini wakapanga kujenga timu ya maana.

Midfield itakaa vizuri wala sina wasiwasi nayo. Kwa upande wa beki, Kapombe na Zimbwe wawe kwenye kwenye rotation, mbadala wao wapo tena wenye viwango, hakuna tena visingizio. Tusikariri kikosi na tujenge ujasiri wa kuweka watu benchi. Kwa kipa tuna Camara, tuna Lakred, tuna Abeid....Mungu atupe nini tena jamani?

Pungufu moja kubwa ambalo linaweza kuja kuicost timu ni uhaba wa striking force. Freddy hawezi kwenda na speed ya hii timu. Imagine Yanga ina options kama Musonda, Dube, Baleke, Mzize, nk. ila Simba hata option ya kwanza bado ina mashaka. Nitampa muda zaidi kidogo Mukwala ila hajaonyesha kama ni katili na mtumiaji mzuri wa nafasi.

Ushauri wangu, kama muda unaruhusu arudi sokoni atafute striker wa maana, atanishukuru baadae. Simba ya sasa ni nzuri sana ila itakwamishwa na ukosefu wa mshambuliaji katili ambaye mambo yakiwa magumu ana uwezo wa kuibeba timu katika migongo yake. Ukosefu wa mshambuliaji tishio utawapa pressure sana mabeki. Wote tuliona leo ilivyofika dakika ya 60 jinsi beki ilivyochoka hadi wakaanza kupoteza umakini na mipira.

Nyongeza, Mutale ana speed nzuri na uwezo wa kupiga chenga ila hana good touch na pia hana good timing kusoma kwa haraka movement na maamuzi ya mtu anayemkaba. Hilo inabidi lifanyiwe kazi haraka, anaanza kunipa wasiwasi kama anafuata nyayo za Saido.
 

van dee

Mgeni
Jun 22, 2024
7
4
5
Kuhusu striker Mimi naona tupo vizuri...shida IPO kwenye winga anaejua kuforce...mwanzoni tulikuwa na kibu ila kwa saivi amepungua kiwango kidogo..kwa upande wa balua namwenyewe bado hajakidhi vigezo vya winga wanavyotakiwa...ila Kuna kina awesu, karabaka nao Hawa pia bado sana..kwa upande wa watani angalia mtu kama nzengeli, au pacome ni watu ambao wanauwezo wa kuforce na kulipa timu ushindi hata muda ambao haujatarajiwa..KIUFUPI TUTAFUTE WINGA ZINAZOWEZA KUTEMBEA NA BOLI SIO KUCHEZEA BOLI.✍️🦁