Mpira ni zaidi ya hamasa za viongozi nje ya uwanja

Feb 7, 2023
61
36
5
Nimetoka kutazama mechi ya Al Alhly dhidi ya Mamelod Sundown, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Nikiwa naangalia hii mechi yenye hadhi ya fainali ghafla nikakumbuka kwamba hii ndo michuano wanayoshiriki Simba pia.

Simba ambao wao wamewekeza zaidi kwenye hamasa za nje ya uwanja huku wakiwa wamesahau kwamba timu yao inahitaji quality players ili kushindana na miamba kama Mamelod, Al Ahly, Wydad, Raja na Petro de Luanda.

Ukiangalia wenzetu wamewekeza zaidi ndani ya pitch, kuleta wachezaji wenye ubora mkubwa na sio propaganda za viongozi nje ya uwanja.

Mamelod Sundown yupo ugenini lakini anamiliki mpira kama kawaida, anamshambulia Al Ahly bila kuhofia yupo ugenini, hii yote ni vile wamejipanga zaidi ndani ya uwanja.

Lakini timu za hapa kwetu Simba na Yanga wao utawasikia malengo yetu kufika nusu fainali lakini Ukiangalia nini wamewekeza kwenye timu hakuna zaidi ya maneno ya propaganda, THAT'S A SHAME

Mpira hauchezwi mdomoni, tuchukue case study ya mchezo wa leo kati ya Mamelod dhidi ya Al Alhly, alafu rudi kwenye timu yako jaribu kupima mzani, utakuja kugundua bado tuna safari ndefu sana kufika nchi ya ahadi. 20230226_001407.jpg