Mputu atundika Daluga rasmi

Feb 7, 2023
61
36
5
Kiungo mkongwe wa klabu ya Tp Mazembe Tresor Mputu ametangaza rasmi kuachana na mpira wa miguu baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo na timu yake ya taifa DR Congo 🇨🇩.

Kiungo huyo fundi mwenye miaka 37 alishawahi kwenda kufanya majaribio ndani ya kikosi cha Arsenal lakini aliamua kurejea tena Mazembe, kwasababu aliamini hakuna klabu bora duniani kuzidi Tp Mazembe inayopatikana jiji la Lumumbashi.

Mafanikio yake makubwa aliyopata ni pamoja na;
2x CAF champions league
2x CAF super cup
1x CAF confederation cup
Mfungaji bora wa muda wote wa CAFCL akifungana na Mohamed Aboutrika wa Al Alhly
2007 CAF champions league top scorer
2009 African Nations championship player of the Tournament.

20230210_133006.jpg
 
  • Like
Reactions: Bangala