Mtibwa, Polisi kuamua krismasi leo

mhindi

Mgeni
Nov 29, 2021
17
6
5
Tanzania
LEO kwenye Uwanja wa Gairo Morogoro, Mtibwa Sugar na Polisi Tanzania zitakuwa zikichuana kutafuta matokeo ambayo yatazifanya kula sikukuu ya Krismasi bila mawazo.

Hiyo ni kutokana na pointi za timu hizo mbili na nafasi zilipo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambapo Polisi ipo nafasi ya nne na alama 15 ikihitaji ushindi ili kufikisha pointi 18 na kula Krismasi ikiwa nafasi ya tatu.

Hivyo hivyo, Mtibwa iliyoko mkiani na alama sita, itaingia uwanjani kutafuta ushindi ambao utaifanya ifikishe pointi tisa na kupanda hadi nafasi ya 11 na kula Krismasi bila ‘stresi’ za kushuka daraja.

Hayo yote yataamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika na makocha wa timu zote mbili wameeleza kujipanga kuondoka na ushindi.

Kocha msaidizi wa Mtibwa, Awadh Maniche alisema wameandaa vizuri kikosi wakitarajia ushindi.

“Tunatambua ubora wa wapinzani wetu, tumeandaa vizuri kikosi na tupo tayari kwenda uwanjani kutafuta ushindi muhimu kesho (leo),” alisema Maniche.

Naye Malale Hamsini wa Polisi alisema kuwa timu ipo Morogoro tangu juzi na hiyo ni katika kuonyesha ni namna gani wamejipanga kushinda mechi hiyo.

“Tulifika Morogoro mapema baada ya mechi na Dodoma Jiji, tumefanya mazoezi mepesi na sasa tupo tayari kuwakabili Mtibwa,” alisema Malale.

Michezo miwili iliyopita ya ligi Mtibwa ilishinda moja dhidi ya Biashara (2-0) na kutoa suluhu dhidi ya KMC, huku Polisi ikishinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na sare 1-1, dhidi ya Dodoma Jiji.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MTIBWA YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 1-1 GAIRO

Wenyeji, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Shabiby huko mjini Morogoro.
Vitalis Mayanga alianza kuifungia Polisi dakika ya 14, kabla ya Datius Peter kujifunga dakika ya 57 kuipatia Mtibwa bao la kusawazisha.
Kwa sare hiyo, Mtibwa inafikisha pointi saba na inaendelea kushika mkia, wakati Polisi imetimiza pointi 16 na kurejea nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi 10 sasa.
 

Attachments

  • gairo.PNG
    gairo.PNG
    513.1 KB · Somwa: 0