MTIBWA SUGAR YAILAZA COASTAL UNION 1-0 MKWAKWANI .

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
1640715319877.png

TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Bao pekee la Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Salum Kihimbwa kwa penalti dakika ya 27.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 10 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 11.