Muhimu alama tatu kwanza,timu kutocheza vizuri sio muhimu kwa sasa

Feb 7, 2023
61
36
5
Simba wamepata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Vipers katika mashindano ya klabu bingwa Afrika ugenini.

Ushindi huo unawafanya kufikisha alama 3 wakiwa nafasi ya tatu, Simba walihitaji zaidi matokeo haya kuliko kuonyesha kiwango bora ili kuweza kurejesha morali ndani ya timu.

Kuhusu kutocheza vizuri nafikiri mwalimu Robertinho na benchi lake la ufundi wana kazi kubwa ya kufanya kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo kiungo,kujilinda pale timu ikipoteza mpira na kutumia nafasi.

Ushindi wa leo unaleta picha kwamba Simba bado wana nafasi ya kwenda hatua inayofuata huku akiomba Horoya apoteze mchezo wake na Raja usiku huu.

Wakati yeye akitegemea kuvuna alama tatu nyingine nyumbani dhidi ya Vipers.

Kongole kwa wachezaji, viongozi na benchi la ufundi kila mtu kacheza kwenye nafasi yake kuhakikisha timu inapata ushindi leo.

20230225_220614.jpg