MZEE MPILI: NIKO TAYARI FIGO YANGU IUZWE PESA APEWE AZIZI KI ABAKI YANGA

DeviMitupio

Mgeni
May 27, 2024
9
4
5

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga, Haji Omary maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa yuko radhi kutoa figo yake iuzwe ili achangie pesa kumbakisha klabuni hapo kiungo mshambuliaji wao, Stephanie Aziz Ki.

Aziz Ki ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu, anatajwa kuwa mpaka sasa bado hajasaini mkapata mpya na huenda akatimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu kwani vilabu kama Mamelodi, Al Ahly, ES Tunis na vingine vingi vimeweka mkwanja mrefu kumgng’oa Jangwani.

“Kuna wakati natamani timu yangu isicheze Klabu Bingwa kwa Masuala kama haya yani Magwiji wa Soka barani Afrika wanapenda sana kutukalia kooni, kiukweli Aziz mpira anaujua ila hio hela anayotaka ni nyingi sana inafika muda natamani kuuza figo ni vile tu wateja hakuna.

“Ushauri wangu kwa Viongozi wa Klabu kama Mchezaji ataendelea kusisitiza kupewa hio hela basi waachane nae, wasifanye maamuzi ya kuiumiza Klabu huenda riziki yetu imeishia hapa,” amesema Mzee Mpili, Mwanachama na Shabiki wa Klabu ya Yanga.

 
  • Like
Reactions: Amir

Zola

Mgeni
May 29, 2024
1
1
5
Kiukweli hatuna namna ya kufanya kwasababu vilabu vilivyoweka pesa ni vikubwa na uchumi wao uko juu ila hapa ndio muda wetu kujitathimin na kupambana na vilabu hivi kwa kujipanga na sisi kuweza kufikia uwezo huo hata wa kumbakisha mchezaji tumefikia hatua kubwa kupandisha vilabu vyetu kwenye chati kubwa afrika hivyo ni muda pia wa kutafta uwekezaji zaidi ili tuweze kuwamiliki wachezaji wakubwa na kubeba mataji makubwa kuleta mageuzi na ushindani katika mchezo tusiishie tu kushangilia nusu fainal na robo fainal twende fainal na ikiwezekana tubebe kabisa mataji na kuandika historia hasa kwa ukanda wa kwetu iivyo kwa wachezaji wa nje kutamani ligi yetu basi hata vilabu vya nje ifike navyo vitambue kuwa Tanzania kuna vilabu vikubwa vyenye upinzani mkubwa tusiishie kuwatengeneza wachezaji wanakuwa wakubwa halafu tunapokonywa hata kwa hela nyanya eti kisa sisi ni wanyonge hatuna pesa za kuwalipa ifike mahala na sisi tubisane nao sokoni tukifika hapo basi mataji tunayaleta Tanzaniam
 
  • Like
Reactions: Amir

Sereweji

Mgeni
May 29, 2024
5
3
5
Kuna maisha baada yakutoa figo kama pesa haipoo muacheni tuu aende hakika kila kitu kinazaid yake nahisi atakuja mchezaji mwenye makal zaid ya azizi
Mzee mpili punguza bangi