Ni nini faida ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande?

tototundu

Kaka Mkubwa
Nov 26, 2021
23
21
6
Kwa ujumla dhamana za fedha (hisa, hatifungani, vipande) ni rasilimali ambazo zinagawanyika na ni rahisi kuziuza kwa kiurahisi. Kutokana na 3 urahisi huo, dhamana zinaweza kuwekwa rehani kwa ajili ya kupata mkopo kutoka taasisi za fedha. Wawekezaji kwenye hisa wanapata gawio ikiwa kampuni itakuwa imepata faida. Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa.

Ongezeko la thamani ni tofauti ya bei ya kununulia hisa na bei ya kuuzia. Ikiwa bei ya kuuza ni ndogo kuliko bei ya kununulia, mwanahisa anapata hasara. Uwekezaji kwenye hisa hauna uhakika wa gawio kwa sababu gawio linategemea faida ya kampuni. Kwa upande wa hatifungani, riba inayolipwa inajulikana tangu mwanzo kwa sababu ni asilimia ya deni lote. Riba inayolipwa inaweza kuwa ya kubadilikabadilika au isiyobadilika.

Wawekezaji kwenye hatifungani wanaoamua kukaa nazo hadi zitakapopevuka wanajua kiwango cha faida yao tangu wanapowekeza. Hatifungani pia zina ongezeko la thamani. Kwa upande wa vipande, faida inategemea aina ya mpango. Vipande ni sehemu ya umiliki kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Tofauti na hisa vipande vinajumuisha mseto wa uwekezaji wa vitega uchumi mbali mbali ambavyo fedha zilikusanywa kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja zinawekezwa.

Kama ni mapango wa kukua, mwekezaji anategemea kufaidika kutokana na kukua kwa thamani ya vipande. Wawekezaji wanatakiwa kujua kuwa bei ya vipande inabadilika mara mwa mara. Kama mpango wa uwekezaji wa pamoja ni wa mapato, mwekezaji anafaidika kutokana na mgao wa mapato ya mpango huu.