Nitasimama na wachezaji wangu hadi kufa- Kocha Mkuu wa Uhispania, Luis Enrique.

kamakawa

Mgeni
Nov 4, 2022
60
57
5
Nitasimama na wachezaji wangu hadi kufa- Kocha Mkuu wa Uhispania, Luis Enrique.

Enrique aliwatetea wachezaji wake na mtindo wake wa kucheza soka baada ya kuondolewa kwenye Kombe la Dunia la Qatar kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 bora dhidi ya Moroccojana (Jumanne).

Uhispania walidhibiti zaidi ya asilimia 75 ya mpira kwenye mchezo huo, lakini walishindwa kupata shuti lililolenga lango kutoka kwa mchezo wa wazi ndani ya dakika 120, huku juhudi zao pekee kulenga goli zikitoka kwa vipande vilivyowekwa.

“Nimefurahishwa sana na wachezaji nilionao, nitasimama nao kufa na kupona, nimewachagua na nawapongeza kwa namna walivyofanya na kwa Kombe la Dunia,” alisema Enrique.

Kinachotukera ni kuondoka kwenye Kombe la Dunia,” aliongeza kocha huyo ambaye hakuwa na malalamishi kuhusu kushindwa.

"Tulitawala mchezo, lakini tulikosa bao: safu ya kiungo ilidhibiti mpira, unaweza kutukosoa kwa kutotengeneza nafasi, lakini Morocco walilinda vyema," alisisitiza.
82085a2a-ec05-4da5-ac2c-e7dcb9c5b22a.jpg