Pep aendeleza ubabe kwa Arteta

Feb 7, 2023
61
36
5
MBINU MBINU MBINU.....

Nani aliamini leo Guardiola ataingia na back 3, huku wingback wake wakiwa Mahrez na Grealish wakiwa na kazi kubwa ya kuwakabili Martinell na Saka, lakini Pep amefanya hivyo na kufanikiwa.

City waliingia na 3-2-4-1,kwenye back 3 Dias,Walker na Ake juu yao kuna Rodri na Silva ( double pivot) huku washambuliaji 4 nyuma ya Halaand ni Gundogan,De bruyne Mahrez na Grealish.

Nini Pep alitaka kwenye mfumo huo ni kuhakikisha eneo la katikati ambalo Arsenal wanalitumia zaidi anakuwa na idadi ya viungo wengi ambapo Arsenal wakati wanamiliki mpira wanakuwa kwenye 3-2-2-3,Zichenko akiungana na Jorginho kati.

Pep kwanza alihakikisha Zichenko na Jorginho wanafanyiwa Man marking na Grealish na Mahrez ili kuwanyima Arsenal uhuru wa kutengeneza mashambulizi kupitia kati,huku wakiwalazimisha kufanya makosa kwenye eneo lao( PRESSING)

City walifanikiwa kupora sana mipira(TURNOVER)kwa Arsenal na kutengeneza nafasi za magoli.

Bernado Silva kwenye karatasi alikuwa kama kiungo wa kati lakini muda mwingi wa mchezo alicheza kama beki wa kushoto kumsaidia Ake dhidi ya Saka.

Pep ameendelea kutoa darasa kwa Arteta,mechi ya sita anatoa dozi kwa mwanafunzi wake.

City top of the table

FT: ARSENAL 1-3 CITY.20230216_013036.jpg
 
  • Like
Reactions: Kriss and Joan