Playmaker Ni Nani Kwenye Soka...??

ChichaMandi

Mgeni
Dec 15, 2022
65
71
5
Katika mazingira Mengi,kuna uelewa tofauti Sana kwq Baadhi ya juu ya watu Neno Playmaker na Namna linatumika Kwenye Mpira,kikwetu.playmaker anachukuliwa mtu anayetengeneza assits nyingi na Nafasi Nyingi na ndio kigezo kikubwa Cha Kumpima playmaker.Ni Nani Maana Halisi ya Playmaker??Ni Lazima playmaker awe na assists Nyingibna chances Nyingi??Ni Kigezo Halisi.?? Jibu Ni hapana.

Playmaker Kwenye Mpira sio mtu anaye assists na Kutengeneza Nafasi Pekee,kwenye Mpira playmaker ni Mchezaj anayeuendesha Mchezo yaani Anayeamua timu Icheze Vipi.Playmaker wanahusika Zaidi Katika part ya kushambulia na kuzuia timu Zao, Sababu Hawa huhusika Zaidi Katika moves za Pasi iwe Kwenye Kutoka Kwenda kushambulia au Kutoka Kwenye kuzuia.kiufupi playmaker Anaweza Kabisa asiwe na assists nyingi na Wala asiwe na chances creation Nyingi, kulingana na Namna kocha anatengeneza mbinu zake.

Playmaker pia wanagawanyika Wapo wale ambao wanakuwa Chini Zaidi (deep lying playmaker) Wapo ambao wanakuwa juu Zaidi (advanced playmaker au classic #10) na pia Wanaweza kuwa Kwenye Maeneo mengin kama Mawinga,centre Midfielder kulingana na mkufunzi.

Hivyo basi kigezo Cha Assists na chances kinaweza kisiwe Kizuri Sana Ikiwa hatutoangalia Zaidi Namna timu inatengeneza mbinu zake na moments za wao Kupata Mabao.Kama tutataka kuwapima playmaker Kwa Kutumia kigezo Cha Assists na Nafasi za Magoli waliotengeneza basi ni Lazima tuguse mbinu za timu kiujumla Kabla ya yote.
 
  • Like
Reactions: SAFARI