Quality imeamua Mechi ya Simba Jana.

Feb 7, 2023
61
36
5
Ubora wa kikosi cha Raja dhidi ya Simba ndo ulioamua matokeo yale pale kwa Mkapa.

Walicheza very direct wakati wanamiliki mpira pasi ya kwanza ya pili wapo golini kwa Simba,walifanya Movements za kuifungua sana safu ya ulinzi ya Simba.

Inonga mara nyingi alikuwa anatolewa kwenye eneo lake,mfano mzuri goli la kwanza ata la tatu pia,waliifanya timu nzima ya Simba iwe wazi wakati wanamiliki mpira.

Raja wametoa darasa kwa Simba kwamba ubora wa kikosi unahitajika sana ili kufanikiwa kimataifa na sio hamasa za nje ya uwanja peke yake.

Simba wanatakiwa kushinda mechi zao mbili dhidi ya Vipers ili kurudisha matumaini ya kufuzu robo fainali.

Kwa mara ya kwanza Simba amepigwa kwa Mkapa kwenye klabu bingwa Afrika toka 2003, tena amefungwa kipigo heavy.20230219_093801.jpg