Ratiba Ya CAF Zawabana SIMBA, YANGA,AZAM Na COASTAL Usajili Wao

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
254
356
25
CAF Imeonesha kalenda ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, huku ikionekana kuwa ratiba ya msimu huu imebana, hivyo muda uliopo ni mchache sana kwa usajili.

Tanzania imefanikiwa kupata nafasi ya kuingiza timu nne kwenye mashindano ya Kimataifa, Yanga SC, Azam FC watakipiga Ligi ya Mabingwa, huku Simba SC na Coastal Unioni kukipiga Shirikisho.

Kwa mujibu ya ratiba ya CAF inaonesha mchakato wa kuanzia mwanzo wa mashindano hayo hadi siku ya fainali ya msimu wa 2024/2025, inaonyesha kuwa hatua ya awali mechi zake zitaanza Agosti 16 na 18, huku hatua ya makundi ikitarajiwa kupigwa Oktoba hadi Desemba 2024.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa fainali italazimika kuwa Mei mwaka 2025 mfumo ukiwa uleule wa nyumbani na ugenini.

Hii ina maana kuwa timu za Azam na Coastal Union ambazo zinaonekana kuwa zitaanzia hatua ya awali zinatakiwa kuhakikisha zimekamilisha usajili wake hadi Julai 20, huku zile za Simba na Yanga ambazo zitacheza hatua ya kwanza zikipewa kutoka Julai 21 hadi Agosti 31 kuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha usajili wake Caf.
 

Hagai paul

Mgeni
Jun 5, 2024
2
1
5
Kila la kheri timu zetu zote katika usajili tupate wachezaji wazuri ambao watatufikisha mbali.maana kufanikiwa kwa vilabu vyetu ni kufanikiwa kwa Tanzania.
 
  • Like
Reactions: Steve mabena

T J

Mpiga Chabo
May 15, 2024
5
0
0
Sijajua kwa simba, azam, na costal ila yanga naona wako smart sana pia wanania ya kufanya vzr hvy watakamilisha chap
 

Saidy

Mgeni
Jun 5, 2024
42
10
5
Yote kwa yote, usajili isiwe kikwazo kikubwa. Cha msingi watumie pesa kufanya usajili na sio kusubiria wale wachezaji walioachwa na vilabu vingine. ili kufanikisha haraka ni kumnunua mchezaji ata kama alikuwa na mkataba kwenye timu anayochezea. Ndio maana nikasema pesa itumike ili kufanikisha zoezi hilo haraka 🙏
 

francosjr

Mgeni
May 2, 2024
7
4
5
Kila lakheri timu zetu,,,tuweke uzalendo mbele kwa kuzisapoti timu zetu ili kulifikisha soka la tanzania mbali zaidi
 

Sir tenge

Mgeni
Jun 5, 2024
11
4
5
Uzalendo bila mipango ni kupoteza muda,halafu hayo mambo ya uzalendo ndio yanayofanya mpira wetu usisogee na kupiga hatua