Ronald Araùjo kiboko ya Mawinga wasumbufu

Feb 7, 2023
61
36
5
Jana kwenye El Classicò tulishuhudia beki kisiki wa Fc Barcelona Ronald Araùjo akimuweka kwenye mfuko winga hatari wa Real Madrid Vini Jr.

Araùjo alipewa kazi maalum na Xavi ni kuhakikisha anamfanyia Marking Vini asilete madhara kwa upande wao.

Vini Jr ni mchezaji mwenye kasi sana hivyo anahitaji kufanyiwa Marking ya karibu zaidi hatakiwi kupewa nafasi ya kupokea na kugeuka na mpira it's a risk.

Mara nyingi Xavi anamtumia Araùjo upande wa beki wa kulia pale anapokutana na timu yenye winga mwenye kasi na msumbufu,kwa sababu Araùjo ana nguvu, kasi na uwezo wa kupambana 1v1.

Jana Real Madrid walipoteza kwa goli 1-0 wakiwa kwenye dimba lao kwa mara ya kwanza baada ya miezi 11,mara ya mwisho kupoteza ilikuwa dhidi ya Chelsea kwenye Uefa.

Lakini pia Jana Madrid walishindwa kupiga shuti lililolenga lango,mara ya mwisho kushindwa kufanya hivyo ni 2010.20230303_010134.jpg