RONALDO KATEMA NYONGO UKO MANCHESTER UNITED

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
“Hakuna kilichobadilika hapa tangu Sir Alex alipoondoka. Nilipoamua kurejea Manchester United, nilifuata moyo wangu. Sir Alex Ferguson aliniambia: ‘Haiwezekani wewe kwenda Man City!’. Na nikasema: ‘Sawa, bosi’… kwa hiyo, nilirudi. Lakini hakuna kilichobadilika hapa. Maendeleo ni SIFURI”.

"Ninaipenda Manchester United, ninawapenda mashabiki, daima wako upande wangu. Lakini kama klabu wanataka kufanya mambo kuwa tofauti… inabidi wabadilishe mambo mengi sana.”

"Nadhani mashabiki wanapaswa kujua ukweli. Naitakia klabu mema zaidi. Ndiyo maana nimekuja Manchester United. Lakini kuna baadhi ya mambo ndani ambayo hayatusaidii (sisi) kufikia kiwango cha juu kama City, Liverpool na hata sasa Arsenal."

"Sir Alex Ferguson anajua vizuri kuliko mtu yeyote kwamba klabu haiko kwenye njia wanayostahili kuwa. Anajua. Kila mtu anajua. Watu ambao hawaoni hilo ni kwa sababu hawataki kuona; ni vipofu.”

"Nilihisi baadhi ya watu hawanitaki hapa [Manchester United] sio tu mwaka huu lakini mwaka jana pia."

Cristiano Ronaldo kuhusu Ten Hag:

“Sina heshima kwake kwa sababu haonyeshi heshima kwangu. Ikiwa huniheshimu, sitawahi kukuheshimu kamwe.”
5a6e69cb-f502-4547-adb0-cdb7d7164813.jpg