SABITZER KUSAJILIWA NA UNITED.?

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
SABITZER KUSAJILIWA NA UNITED.?

Mshauri wa Marcel Sabitzer Roger Wittmann amesema kuwa wanamuona Sabitzer akiwa na kiwango kama alivyokuwa RB Leipzig ya Ujerumani🇩🇪 ndani ya Manchester United.

Wittmann anasema kuwa wanafuraha sana kumuona Sabitzer akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu ndani ya United.

Wittmann aliongeza kwa kusema nini kitatokea kwenye majira ya joto - tutaona wakati ukifika.

Roger Wittmann🗣️: "Kwenye klabu ya Manchester United tunamwona Marcel kutoka Leipzig tena. Nina furaha sana kwake. Nini kitafuata majira ya joto? Tutaona wakati ukifika."

NB: Ikumbukwe kuwa klabu ya Bayern Munich waliwaambia United kuwa wapo tayari kumuuza moja kwa moja kwa ada ya Pauni Milioni 20 (£20m).

49141A48-3C28-4EAA-9168-3F850A3506E5.jpeg
 
  • Like
Reactions: kamakawa