Scouting ya Simba imefeli kufanya sajili nzuri kwa misimu miwili sasa.

Feb 7, 2023
61
36
5
Miezi 8 nyuma Kassim Dewji alisema kuwa Simba SC haitumi njia sahihi kufanya usajili na wanahitaji mtaalam kwenye eneo hilo. Lakini alionekana anatengeneza migogoro.
Leo ukiangalia usajili uliofanywa na Simba SC kwenye madirisha 2 yaliyopita zaidi ya 45% umefeli.

Ukiangalia kuna ukweli ndani yake, Simba wamesajili wachezaji wengi wa kigeni ambao wamekuwa hawatumiki Outtara,Okwa,Akpan na wengine wengi ambao wamekuja hapa lakini wameshindwa kuonyesha ubora wao.

Hii ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanafanya sajili zenye ubora mkubwa na manufaa kwa timu yao.

Unaweza ukawa unajiuliza ni huo udalali unaofanywa na viongozi kusajili wachezaji ambao hawajatumika kwa muda mrefu au ni kweli wameshindwa kufanya scouting nzuri.

Ukiangalia watani zao yanga wamekuwa tofauti kidogo wanasajili wachezaji kwa matakwa ya kocha,lakini pia ni mchezaji mwenye uwezo wa kupambania namba na uwezo mkubwa uwanjani.

Ni wakati sasa kwa Uongozi na Scouting team ya Simba kujitafakari wanafeli wapi kwenye usajili kwa miaka ya hivi karibuni, toka afariki Zakaria Hanspope Simba wamekosa mtu sahihi kwenye usajili.20230224_093400.jpg
 
  • Like
Reactions: McRay