Sergio Aguero: Mshambulizi wa Barcelona atangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 33 kutokana na ugonjwa wa moyo.

Mfungaji bora huyo wa Manchester City, ambaye alihamia Barcelona kwa uhamisho wa bure msimu wa joto, alilazimika kubadilishwa wakati timu yake ikitoka sare ya 1-1 na Alaves mwezi Oktoba baada ya kupata msaada wa matibabu uwanjani kutibu maumivu ya kifua na kizunguzungu. Mshambulizi huyo wa Argentina alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya moyo na baada ya hapo akawekwa nje kwa miezi mitatu. Hata hivyo, Aguero hakurejea uwanjani kabla ya kutangaza Jumatano huko Nou Camp kwamba maisha yake ya uchezaji yamekamilika. Aguero kwa hisia kali alisema: "Mkutano huu ni wa kuwasilisha kwamba nimeamua kuacha kucheza soka. “Ni wakati mgumu sana, uamuzi nilioufanya nimeuchukua kwa ajili ya afya yangu, ndiyo sababu kuu, kutokana na tatizo nililokuwa nalo mwezi mmoja na nusu uliopita."Nilikuwa mikononi mwa wafanyikazi wa matibabu ambao wamefanya vizuri na wameniambia jambo bora ni kuacha kucheza."Kwa hivyo nilifanya uamuzi huo takriban wiki moja iliyopita na ninataka kumwambia kila mtu nilifanya kila linalowezekana kuwa na matumaini, lakini hakukuwa na mengi sana."
 

Attachments

  • aguero.PNG
    aguero.PNG
    813 KB · Somwa: 0