Simba bila chama yaambulia pointi moja

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Simba Ikicheza bila Chama imeambulia pointi moja mbele ya Singida Big Stars mchezo uliochezwa jana katika dimba la Liti Singida.

Chama alifungiwa michezo mitatu na (TFF) kutokana na kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani katika mchezo wa Ligi Kuu, kwenye mechi yao dhidi watani wao wa jadi Yanga.
Simba imeendelea kuongeza gape la pointi 5 dhidi ya watani wake Yanga baada ya kuambulia pointi 1 na kua na pointi 18 huku singida wakiwa na pointi hizo hizo 18 kwenye mechi yao ya jana, Simba akishika nafasi ya 3 na Singida nafasi ya 4.

Singida ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 kutoka kwa winga Deus Kaseke aliyemalizia krosi ya Said Ndemla.

Dakika ya 58 Simba ilifanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa Banda, Na kufanikiwa kuokoa point 2 na mechi kumalizika kwa sare ya 1-1
 
  • Like
Reactions: jamal