Simba kufa, kupona leo

Feb 7, 2023
61
36
5
Simba leo jioni atashuka dimbani akiwa mgeni wa Vipers katika dimba la St. Mary's nchini Uganda.

Katika mchezo wa leo Simba ataingia akiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Horoya na Raja huku akiwa hajafunga goli lolote kwenye michezo hiyo.

Hivyo Simba leo wataingia huku matokeo watakayokuwa wanahitaji zaidi ni ushindi ili aweze kurudisha matumaini ya kufuzu robo fainali.

Wakati huo mwenyeji wake pia Vipers atahitaji matokeo ya ushindi ili afikushe alama nne ambazo zitamsaidia kusogea kwenye nafasi za juu.

Ukiangalia kikosi cha Simba kina ubora na uzoefu mkubwa tofauti na Vipers hivyo Simba wanapewa nafasi ya kushinda mchezo wa leo, japo kwenye mechi za hivi karibuni wamekosa kuonyesha ubora wao.

Kumbuka ushindi wa Simba utaongeza hali ya kujiamini kwao na mashabiki, lakini wakipoteza itakuwa mbaya zaidi kwao kuelekea muendelezo wa ligi kuu na hata michuano ya Afrika.

Je, unaiona wapi leo Simba dhidi ya Vipers nini wafanye waweze kupata ushindi?20230225_154454.jpg