Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Nyumbani
Majukwaa
Story Mpya
Tafuta Majukwaa
Story Mpya
Posti Mpya
Posti Mpya za wasifu
Vilivyofanyika
Wanachama
Wanaotembelea kwa sasa
Posti mpya za wasifu
Tafuta Posti za wasifu
Ingia
Jiunge
Tafuta
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Tafuta vichwa vya habari tu
Kutoka kwa:
Menu
Install the app
Install
Reply to thread
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Simba Sports Club Thread
JavaScript is disabled. For a better experience, please enable JavaScript in your browser before proceeding.
You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly.
You should upgrade or use an
alternative browser

Message

Simba ya Kimataifa: Kwani nyie wenzetu mnafeli wapi?

SIMBA imeanza vizuri hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi ndio pekee waliobaki wakiiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa, na mashabiki kadhaa wa Simba walisikika wakihoji kwa furaha: “Kwani nyie mnafeli wapi?”

Wawakilishi wengine wa Tanzania – Azam, Yanga, Biashara, Mafunzo na KMKM – walitolewa mapema kabisa.

Matokeo hayo ni mazuri na muhimu kwa Simba ikielekea kucheza mechi yake ya pili ya michuano hiyo dhidi ya USGN ya Niger, Februari 20, mwaka huu.

Katika mchezo wa juzi, bao la kwanza la Simba lilifungwa na Pape Ousmane Sakho dakika ya 12, lilikuwa ni bao kali lililofungwa kwa staili ya mbinuko ‘Acrobatic Style’ akiitendea wema krosi kutoka Magharibi mwa uwanja iliyopigwa na Shomari Kapombe.

Simba walianza kwa kumiliki mpira katika dakika mbili za mwanzo na kutengeneza shambulizi kupitia kwa Meddie Kagere.

Ndani ya dakika 5 za kwanza, Simba walikuwa wamepiga krosi sita na kutengeneza kona moja.

Lakini dakika ya 14, Asec walitengeneza shambulizi na Anicet Allain Oura akapiga shuti lililopaa juu ya lango.

Dakika ya 22, Kagere alijaribu kufunga bao na nusura afunge, lakini shuti lake aliligongesha mwamba wa chini.

Dakika ya 25, Simba walipata kona nyingine lakini walishindwa kuitumia vizuri. Dakika 31 Karim Konate wa Asec, alipiga shuti langoni lililodakwa na Aishi Manula.

Dakika ya 36, Pape Sakho anakaa chini na kuonyesha ana maumivu, na dakika ya 40 anaonekana ameshindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake inachukuliwa na Mzamiru Yasini.

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, dakika ya 45 Peter Banda anakosa bao akiwa amebaki yeye na kipa. Shuti lake linapaa juu la lango na kuacha mashabiki wakishika midomo.

Dakika 45 za kwanza, zilimalizika kwa Simba wakiwa wanaongoza bao 1-0.

Kipidi cha pili kilianza kwa spidi ya chini, timu zikiwa zimerejea kama ambavyo zilikwenda mapumziko kwa maana hakuna mabadiliko.

Dakika mbili za kwanza, 45 hadi 47, Asec walitengeneza mashambulizi mazuri moja likiwapa kona.

Dakika ya 60, Asec walisawazisha kupitia kwa Azizi Stephenie, baada ya uzembe na kujichanganya kwa safu ya ulinzi ya Simba. Joash Onyango akipiga mpira unaogonga kiungo wa Asec na mpira kumkuta Azizi aliyemtoka Henock Inonga na kuuweka mpira kwenye kamba.

Dakika ya 68, Sadio Kanoute alitolewa nje na machela na kushindwa kuendelea na mchezo, Yusuph Mhilu alichukua nafasi yake.

Meddie Kagere alitoka na nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco dakika ya 70.

Mabadiliko hayo yaliwapa faida Simba, Mhilu aliwekwa chini dakika ya 76 kwenye 18 na Simba kupata penalti, iliyofungwa na Shomari Kapombe dakika 77.

Bocco on Fire

Ndani ya dakika mbili tangu aingie, anatengeneza nafasi mbili, finishing tamu ya Peter Banda baada ya kazi nzuri ya Bocco dakika ya 78, Simba wakaandika bao la tatu.

Banda alivua shati na kwenda kushangilia, akapewa kadi ya njano.

Dakika ya 86, Banda alikwenda nje nafasi yake ikachukuliwa na Israel Mwenda, huku Bwalya akitoka na Erasto Nyoni akaingia kuchukua nafasi yake katika kile kilichoonekana ni mabadiliko ya kuongeza ulinzi baada ya kuongoza.

[QUOTE="Amir, post: 916, member: 20"] [HEADING=1]Simba ya Kimataifa: Kwani nyie wenzetu mnafeli wapi?[/HEADING] [IMG]https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2022/02/simba-13.jpg[/IMG] SIMBA imeanza vizuri hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Wekundu wa Msimbazi ndio pekee waliobaki wakiiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa, na mashabiki kadhaa wa Simba walisikika wakihoji kwa furaha: “Kwani nyie mnafeli wapi?” Wawakilishi wengine wa Tanzania – Azam, Yanga, Biashara, Mafunzo na KMKM – walitolewa mapema kabisa. Matokeo hayo ni mazuri na muhimu kwa Simba ikielekea kucheza mechi yake ya pili ya michuano hiyo dhidi ya USGN ya Niger, Februari 20, mwaka huu. Katika mchezo wa juzi, bao la kwanza la Simba lilifungwa na Pape Ousmane Sakho dakika ya 12, lilikuwa ni bao kali lililofungwa kwa staili ya mbinuko ‘Acrobatic Style’ akiitendea wema krosi kutoka Magharibi mwa uwanja iliyopigwa na Shomari Kapombe. Simba walianza kwa kumiliki mpira katika dakika mbili za mwanzo na kutengeneza shambulizi kupitia kwa Meddie Kagere. Ndani ya dakika 5 za kwanza, Simba walikuwa wamepiga krosi sita na kutengeneza kona moja. Lakini dakika ya 14, Asec walitengeneza shambulizi na Anicet Allain Oura akapiga shuti lililopaa juu ya lango. Dakika ya 22, Kagere alijaribu kufunga bao na nusura afunge, lakini shuti lake aliligongesha mwamba wa chini. Dakika ya 25, Simba walipata kona nyingine lakini walishindwa kuitumia vizuri. Dakika 31 Karim Konate wa Asec, alipiga shuti langoni lililodakwa na Aishi Manula. Dakika ya 36, Pape Sakho anakaa chini na kuonyesha ana maumivu, na dakika ya 40 anaonekana ameshindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake inachukuliwa na Mzamiru Yasini. Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, dakika ya 45 Peter Banda anakosa bao akiwa amebaki yeye na kipa. Shuti lake linapaa juu la lango na kuacha mashabiki wakishika midomo. Dakika 45 za kwanza, zilimalizika kwa Simba wakiwa wanaongoza bao 1-0. Kipidi cha pili kilianza kwa spidi ya chini, timu zikiwa zimerejea kama ambavyo zilikwenda mapumziko kwa maana hakuna mabadiliko. Dakika mbili za kwanza, 45 hadi 47, Asec walitengeneza mashambulizi mazuri moja likiwapa kona. Dakika ya 60, Asec walisawazisha kupitia kwa Azizi Stephenie, baada ya uzembe na kujichanganya kwa safu ya ulinzi ya Simba. Joash Onyango akipiga mpira unaogonga kiungo wa Asec na mpira kumkuta Azizi aliyemtoka Henock Inonga na kuuweka mpira kwenye kamba. Dakika ya 68, Sadio Kanoute alitolewa nje na machela na kushindwa kuendelea na mchezo, Yusuph Mhilu alichukua nafasi yake. Meddie Kagere alitoka na nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco dakika ya 70. Mabadiliko hayo yaliwapa faida Simba, Mhilu aliwekwa chini dakika ya 76 kwenye 18 na Simba kupata penalti, iliyofungwa na Shomari Kapombe dakika 77. [B]Bocco on Fire[/B] Ndani ya dakika mbili tangu aingie, anatengeneza nafasi mbili, finishing tamu ya Peter Banda baada ya kazi nzuri ya Bocco dakika ya 78, Simba wakaandika bao la tatu. Banda alivua shati na kwenda kushangilia, akapewa kadi ya njano. Dakika ya 86, Banda alikwenda nje nafasi yake ikachukuliwa na Israel Mwenda, huku Bwalya akitoka na Erasto Nyoni akaingia kuchukua nafasi yake katika kile kilichoonekana ni mabadiliko ya kuongeza ulinzi baada ya kuongoza. [/QUOTE]
Verification
Kwani 1 + 1 = ni ngapi?
Post reply
Majukwaa
Maskani ya Michezo na Mikeka
Kijiwe cha Ligi Kuu Bongo
Simba Sports Club Thread
Top
Bottom