SIMBA VS AZAM, mechi nzuri, iliyopungua ladha

Kriss

Mgeni
Nov 4, 2022
102
138
5
SIMBA VS AZAM, mechi nzuri, iliyopungua ladha.

Mpira umechezwa na timu zote kwa ari na hali ya juu sana.

Watazamaji bila shaka walifurahia mchezo, isipokuwa hizi timu zimetupunguzia ladha ya mchezo kwa uchache wa magoli yaliyofungwa, ambapo kwa mashambulizi yaliyofanywa na mchezo ulivyokuwa wa kasi sana, ilifaa sana tuone magoli mengi kwenye mchezo huu wa Simba dhidi ya Azam

Nafikiri Simba SC lile goli la mapema ndio liliharibu mpango wao wote, maana wakalazimishwa kuimbikiza mechi na ndio kitu ambacho Azam walitaka Simba walikuwa wanahama kwa haraka nyuma hasa kwa kutumia fullbacks wao na kuwaruhusu viungo wao watatu washambuliaji kucheza ndani zaidi Chama , Saido na Sakho

Tatizo kwa Simba ni ile mfumo wa kuzuia wanapoporwa Mpiraaa Spaces zipo wazi sanaa Fulbacks wanakua wako juu hamna mtu wa Backup Ukilinganisha na Game intensity Leoo SSC wamefika Sanaa Langoni kwa AZAM Shots Nyingii ,, Sema IDRISSU alikua vizuri

Mechi nzuri kwa jasho kubwa la wachezaji nafikiri Simba kweny final third nikuongeza sharpnes,pass accurate na speed Lakin Simba bila mpira dah😢 Haina namba 6 kabisa unawaza kwann timu kubwa zinaifunga Simba ni coz fullback wote Wana overlap zaidi alafu hamna middle cavorage lakin Azam dah Wana watu finishing,speed,wale fullback waona holding middlefielder yes wametoa walicho nacho🔥

Mfumo wa kocha mbaya sana timu ikiwa na mpira mabeki wanakuwa wachache sana nyuma afu space zinakuwa kubwa hiyo ndo Azam walikuwa wanatumia kama faida na ndo walipopata goli Simba wakiendelea hivi wataruhusu sana magoli

Timu yoyote ikitaka kuwamaliza Simba SC kwa urahisi sana ni kushambulia kwa kupitia kati ya Zimbwe na beki wa kati au kati ya Kapombe na beki wa kati......70% Simba SC wanafungwa kutipia hizo sehemu mbili

Simba haiko vizuri Kwa Mara ya kipindi cha pili wacheza wa Simba wanagonga kugombea mpira Kuna vitu haviko sawa pale klabuni wachezaji wamekua wazito kwenye kutengeneza na kujitengenezea nafasi

Chama na Saido wakianza pamoja Simba inakuwa weak sana kwenye kulinda goli.. Na kiukweli Azam wamecheza kawaida tofauti na mechi 3 zilizopita (2 Yanga) na 1Simba mzunguko wa kwanza..

1677046897043.png