Simba Walikua Bora Eneo Gani Mbele Ya Azam Fc?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
281
396
25
Mchezo mkubwa mchezo ambao umeonyesha maana halisi ya Derby ya Mzizima uhasama wa timu mbili ambazo zinamilikiwa na matajiri wawili wakubwa nchini, mmoja akiwa mmiliki na mwingine akiwa Mwekezaji wa timu hiyo.

Kipindi cha kwanza kilionyesha uhalisia na ubora wa Azam FC kwa msimu huu kivipi, kwa Simba SC kukubali kuwa timu Ya pili kiwanjani kwa kuingia huku wakiwaheshimu Azam FC kuwa wao ni bora zaidi yao na ndiyo maana wachezaji wa Simba SC muda mwingi walikuwa chini wakiwazuia Azam FC.

Azam FC walikuwa bora sana kuanzia kuzuia mashambulizi pamoja na kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma, uwezo wa wachezaji wengi wa Azam FC kwenye kumiliki mpira Iddy Nado, Kipre Junior na Gibril Sillah jambo ambalo liliwapa nafasi zaidi Ya kukabia juu ili kuweza kupunguza hatari kwenye Lango Lao na ilo walishinda kivipi ?

Wachezaji wengi wa Azam FC kwenye eneo la ushambuliaji ni wazuri sana wakiwa na mpira na kama ukiwapa nafasi Ya kuwa na mpira muda mwingi bila presha basi ni rahisi sana kukuadhibu na ilo Simba SC walilitambua na kuamua kukabia katikati zaidi, Azam FC wakifika katikati ya uwanja basi wachezaji wa Simba SC walikuwa haraka zaidi kuwazuia Azam FC, japo kuna nyakati Azam FC walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia, ila kwa upande wa Simba SC baada ya kumiliki mpira waliamua kutumia zaidi maeneo yao ya pembeni kwa kushambulia kwa kushtukiza ila walikosa maamuzi sahihi eneo Lao la mwisho na wakati mwingine walikuwa wachezaji wachache dhidi Ya wengi wa Azam FC.

Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kwa upande wa Simba SC kwanini ? Waliamua kuwa juu zaidi na kukimbia eneo kubwa la uwanja tofauti na kipindi cha kwanza uwepo wa Ladack Chasambi na Edwin Balua ulikuwa wakati sahihi kwao kutokea pembeni huku wakiongeza utulivu wanapomiliki mpira kwenye nusu Ya mpinzani wao, uwepo wa Viungo Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin ilikuwa mwanzo wa kuwapa presha wachezaji wa Azam FC wanapopoteza mpira basi wao walikuwa wa kwanza kuanzisha presha kwa wachezaji wa Azam FC.

Namna magoli yao walivyofunga ni kwa sababu ya presha waliyokuwa wanaweka Fredy Michael akiwa mbele zaidi Ya wenzake kutowapa uhuru Fuentes na Bangala na ilo liliwawezesha kutumia vizuri mipira ya pili iliyokuwa ikidondoka kwenye uso wa lango la Azam FC goli la kwanza la Sadio Kanoute pamoja na David Kameta “Duchu” ilo ndiyo jambo ambalo wachezaji wa Simba SC walilifanya kuwaadhibu Azam FC.

Unapopata nafasi ya kuuchukua mchezo ndiyo wakati wako wa kumuadhibu mpinzani wako lakini ilo kwa upande wa Azam FC walilishindwa kulitumia na hata ilo Kocha Yusuph Dabo amelizungumza, miliki mchezo tumia nafasi unazopata.

Wachezaji wa Simba SC waliamua kujitoa na kujituma zaidi kiwanjani siku ya leo walikimbia sana na walikuwa watulivu walipokuwa na mpira na muda mwingi walifanya maamuzi sahihi wakiwa na mpira, waliachia pasi kwa haraka hakuna Mchezaji aliyekuwa akikaa na mpira muda mrefu huku wachezaji wote wakikaba kwa pamoja na kushambulia kwa pamoja.

Nimevutiwa na “Performance” ya wachezaji vijana kiwanjani kwa pande zote mbili Edwin Balua, Israh Mwenda, Ladack Chasambi na kwa upande wa Simba SC, Pascal Msindo, pamoja na Nathaniel Chilambo kwa Azam FC wamevuja jasho kweli wamepambana wamejituma ni swala la kuwapa muda, nafasi na kuwaamini vijana hao kwa kesho bora.
 
  • Like
Reactions: makombo jr