Taarifa Mpya Kuhusu JOHN BOCCO Kukipiga Ligi Kuu Msimu Ujao Tena

May 27, 2024
14
7
5
Taarifa za ndani zinasema kwamba Bocco anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 154 katika misimu 16 akiipiku rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyekuwa amefunga mabao 153 ndani ya misimu 13 amesajiliwa na JKT Tanzania kama kocha mchezaji.
Kabla ya kutua kwa maafannde hao wa JKT Tanzania John Bocco alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba, hivyo suala la yeye kujiunga na Maafande hao inamaanisha hatokuwa tena sehemu ya benchi la ufundi la Simba.
 
  • Like
Reactions: Ayubu salingwa