TAIFA STARS

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Tanzania yaporomoka viwango vya FIFA.​

Tanzania PIC

Tanzania imeporomoka kwa nafasi moja katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA) kwa mwezi Januari.
Kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka vya Januari vilivyowekwa hadharani jana, Tanzania imeanguka kutoka nafasi ya 131 iliyokuwepo mwishoni mwa mwaka jana hadi nafasi ya 132 ikipishana na Comoro ambayo awali ilikuwa katika nafasi hiyo.
Kufanya vizuri kwa Comoro katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika huko Cameroon mwaka huu, kuimeirudisha nchi hiyo katika nafasi ya 131 na kuichomoa Tanzania ambayo haikushiriki.
Gambia ambao walionyesha kiwango bora na kuishia katika hatua ya robo fainali kwenye fainali za Afcon mwaka huu, juhudi zao zimewalipa kwani imejikuta ikipanda kwa nafasi nyingi na kuwatoa shimoni walipokuwepo awali.
Kutoka nafasi ya 150 waliyokuwepo awali, Gambia wamepanda hadi nafasi ya 125 ikimaanisha wamepaa kwa nafasi 25 zaidi.
Usemi wa chanda chema huvikwa pete, unaweza kutumika pia kwa mabingwa wapya wa Afcon, Senegal ambao wamepaa kwa nafasi mbili kutoka ile ya 20 hadi nafasi ya 18 kidunia huku wakiongoza kwa upande wa Afrika.
Hakuna mabadiliko katika nafasi tatu juu kidunia ambapo Ubelgiji wameendelea kutamba, wakifuatiwa na Brazil katika nafasi ya pili huku wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa ni Ufaransa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BEKI WA TAIFA STARS AFCON 2019 AFARIKI DUNIA.​

AVvXsEjnDFSP8pjkt2A01EHDTX-vNKEsxuhpFR_zrcH7LgLIY9ln2gbnHcvb6Je57c62sqsYCmG-N_XeuoB7itpPqtjtEdnRZ0QV4EUkpAkGsYz4NFR0_vCnxehXGAdy36JtP2dptjPKpD8uKFp-Yy5EEuBZcgYud5GZyhbEFyNdmPhwDLxtXcTB2_1tMFPQ=w640-h632

BEKI wa zamani wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania, Ally Abdulkarim Ibrahim Mtoni ‘Sonso’ (28) amefariki dunia leo wakati akikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Sonso aliyezaliwa Machi 13, mwaka 1993 Jijini Dar es Salaam, alikuwa nje ya Uwanja kwa muda baada ya kuumia mguu kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba Novemba 19 mwaka jana Ruvu Shooting ikichapwa 3-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Chanzo haswa cha kifo cha marehemu au maradhi yaliyokuwa yakimsumbua zaidi ya maumivu ya mguu hakijaelezwa ila mazishi yake yatafanyika nyumbani kwao, Kondoa Magomeni Jumamosi.
Mtoni alisajiliwa Yanga akitokea Lipuli ya Iringa msimu wa 2019-2020 kabla ya kuachwa baada ya kuachwa msimu uliofuata akaenda Kagera Sugar ambako aliichezea hadi msimu huu alipojiunga na Ruvu Shooting.
Ally Sonso alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka 2019.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Mtoni Sonso. Amin.