Taifa Stars

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

KOCHA POULSEN ATAJA KIKOSI TAIFA STARS​


KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poullsen ametaja kikosi cha wachezaji 28 kwa ajili ya mechi za kirafiki kwenye kalenda ya FIFA, ndani yake akijumuisha chipukizi kadhaa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MSUVA MAZOEZINI STARS IKIJIANDAA KUZIVAA SUDAN NA CAR​

CBED8923-C5A3-4073-99FD-402D896F75CD.jpeg


MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Simon MSUVA akiwa mazoezini timu hiyo ikijiandaa na michezo miwili ya kirafiki iliyo katika kalenda ya FIFA dhidi ya Jamhuri yaAfrika ya Kati Machi 23 na Sudan Machi 29 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
344E4A41-1FC1-4EC4-A47D-1892970A4E5A.jpeg

20165497-EA9E-47B5-81EB-7E13201C9414.jpeg
67ED6245-5330-4E73-9597-31E88D5A3FE3.jpeg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

STARS YANG’ARA, YAICHAPA CAR 3-1​

570F39F8-EA5B-4258-9311-649CC55BFF4F.jpeg


TIMU ya Taifa ya Tanzania imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na kiungo Novatus Dismas Miroshi, wa Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Israel dakika ya 10 na washambuliaji, Nahodha Mbwana Ally Samatta wa Royal Antwerp ya Ubelgiji dakika ya 63 na George Mpole Mwaigomole wa Geita Gold ya nyumbani dakika ya 90 na ushei.
Bao pekee la Jamhuri ya Afrika ya Kati limefungwa na mshambuliaji wa Gasogi United ya Rwanda, Christian-Theodor Yawanendji-Malipangou kwa penalti dakika ya 66.
Stars iliyo chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen itacheza mechi mbili zaidi katika kalenda hii ya FIFA, nyingine dhidi ya Botawana Jumamosi na dhidi ya Sudan Machi 29, zote Uwanja wa Benjamin Mkapa pia.
Nazo CAR na Sudan zitamenyana Jumamosi.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kim Polsen akoshwa na bao la Samatta​

paulsen.jpg

KOCHA wa Timiu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Polusen ameonekana kukoshwa na bao la pili kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki, kati ya Taifa Stars dhidi ya Afrika ya Kati liliwekwa kambani na nahodha wa kikosi hiko Mbwana Samatta.

Mchezo huo wa kirafiki wa kalenda ya Shirikisho la Mpira Duniani ‘FIFA’ ulipigwa jana tarehe 23 Machi 2022, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 usiku.

Kim amesema kuwa kwa muda mrefu hajaona aina ile ya bao likifungwa kwa ustadi mkubwa na jinsi lilivyotengenezwa kwa kupigwa pasi kutokea nyuma.

“Wakati wangu bora kwenye mchezo wa leo ni bao la pili, kwa muda mrefu sijaoana aina hii ya mpira na pasi, kwa kweli ulikuwa wakati mzuri.” Alisema Kim

Bao hilo lilifungwa dakika ya 62 ya mchezo ambapo mashambulizi yalianzia kwa mlinzi wa kati Bakari Mwamnyeto na kupigwa jumla ya pasi nne mpaka kumfikia mfungaji.

Aidha kocha huyo aliendelea kusema kuwa amejivunia nafasi kikosi chake kwa kutengeneza nafasi nyingi kwa aina ya timu ngumu kama Afrika ya kati jambao ambao limetia faraja.

“Tumetengeneza idadi kubwa ya nafasi, tumefunga mabao matatu, ukiangalia kwenye kwenye ushambuliaji ninafuraha kutengeza idadi nyingi za nafasi dhidi ya mpinzani kama Afrika ya kati, ambao ni timu nzuri na ngumu na wanacheza vizuri.” Alisema kocha huyo
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

STARS YATOA SARE 1-1 NA SUDAN DAR​

D3D3BA7A-EFAE-4B1B-982E-162F7111A552.jpeg

TANZANIA imelazimishwa sare ya 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Sudan ilitangulia kwa bao la Sadiq Totto mapema tu dakika ya pili, kabla ya Simon Msuva kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 67.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TAIFA STARS YAPANGWA ALGERIA, UGANDA NA NIGER KUFUZU AFCON 2023​

TANZANIA imepangwa Kundi F pamoja na Algeria, Uganda na Niger kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.


MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2023
Kundi A: Nigeria, Sierra Leone, Guinea-Bissau, Sao Tome e Principe or Mauritius.
Kundi B: Burkina Faso, Cape Verde, Togo, Eswatini.
Kundi C: Cameroon, Kenya, Namibia, Burundi.
Kundi D: Misri, Guinea, Malawi, Ethiopia.
Kundi E: Ghana, Madagascar, Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Kundi F: Algeria, Uganda, Niger, Tanzania.
Kundi G: Mali, Kongo, Gambia, Sudan Kusini ,
Kundi H: Ivory Coast (wenyeji), Zambia, Comoro, Lesotho.
Kundi I: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gabon, Mauritania, Sudan.
Kundi J: Tunisia, Equatorial Guinea, Libya, Botswana.
Kundi K: Morocco, Afrika Kusini, Zimbabwe, Liberia.
Kundi L: Senegal, Benin, Msumbiji, Rwanda.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TAIFA STARS KUANZIA NIGER KUFUZU AFCON 2023​


TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa mgeni wa Niger katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
Baada ya Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

TAIFA STARS KUANZA NA SOMALIA KUFUZU CHAN YA MWAKANI​



TANZANIA itaanzia ugenini kwa Somalia katika kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria.
Mechi hiyo itachezwa kati ya Julai 22 na 24, kabla ya timu hizo kurudiana Tanzania kati ya Julai 29 na 31 katika mkoa utakaotajwa baadaye na mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba 2, mwaka huu.
Fainali za CHAN ilikuwa zifanyike Julai 10 hadi Agosti 1, mwaka huu lakini Shirikisho la Soka (CAF) likasogeza hadi mwakani kutokana na kuahirishwa kwa fainali za zilizopita kusogezwa mbele sababu ya Janga la maambukizi ya virusi vya corona.


Ikumbukwe mwezi ujao, Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Taifa Stars itakuwa mgeni wa Niger katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
Baada ya Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

TAIFA STARS KUIFUATA NIGER KWA NDEGE YA KUKODI​



TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakwenda Benin kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
Taarifa ya TFF imesema kutakuwa na nafasi 50 kwa wapenzi wa soka watakaotaka kwenda kuisapoti Taifa Stars ambao watalazimika kulipiadola za Kimarekani 1,000 – kwa taarifa Zaidi wafike TFF.
Baada ya hapo, Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
Bahati nzuri kwa Stars, mshambuliaji wa mabingwa wa England, Manchester City, Riyad Mahrez, Said Benrahma na Sofiane Feghouli hawatakuwepo kwa mujibu wa kocha wa Algeria, Djamal Belmadi wote majeruhi.
Ikumbukwe Stars pia itaanzia ugenini kwa Somalia kati ya Julai 22 na 24 kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria, kabla ya timu hizo kurudiana Tanzania kati ya Julai 29 na 31 nchini na mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

STARS YAWAFUATA NIGER MECHI YA KWANZA KUFUZU AFCON COTONOU​


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imendoka leo kwenda Benin kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger Juni 4 Uwanja wa L'Amitié mjini Cotonou.
Baada ya hapo, Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KIINGILIO TAIFA STARS NA ALGERIA NI SH 3,000 KESHO DAR​



KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast baina ya wenyeji, Tanzania na Algeria ni Sh. 3,000.
Bei hiyo ni kwa majukwaa ya mzunguko, wakati kwa VIP A, B na C ni Sh. 5,000.
Ikumbukwe mechi za kwanza za kuwania tiketi ya Ivory Coast, wakiwa nyumbani Jijini Algiers, Algeria waliichapa Uganda 2-0 na Taifa Stars wakiwa ugenini Jijini Cotonou nchini Benin, walitoa sare ya 1-1 na Niger.
Mbali na Stars na Algeria kumenyana kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, jirani zao, Uganda watakuwa wenyeji wa Niger Jijini Kampala.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

STARS YACHAPWA 2-0 NA ALGERIA DAR KUFUZU AFCON​



TANZANIA imejiwekea ukungu kwenye safari yake ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Ivory Coast baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Algeria usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Algeria yamefungwa na Amir Selmane Ramy Bensebaïni dakika ya 45 na ushei na M. Amoura dakika ya 89 na kwa matokeo hayo Algeria inafikisha pointi sita na kuendelea kuongozi kundi F kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Uganda Jijini Algiers Jumamosi.
Taifa Stars baada ya sare ya 1-1 ugenini na Niger sasa ni ya tatu. Niger baada ya sare ya 1-1 na Uganda leo Jijini Kampala inapanda nafasi ya pili na Uganda sasa inashika mkia.