TANZANITE

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TANZANITE YAICHAPA SOMALIA 1-0 ZANZIBAR.​

AVvXsEgM-4iX2TQsdIbHbiwnz_0dbcE-Nrs-5L3GWYFp3GmcDHYOuit0t-fK1SDvaj3AfhSvlBsPnTOONTeFRVljop4e2lP9ZzlMqh-y0fI4WCF7UNA7zxqoU0-ayUWgOq57JuP1W3aB2RVBOrmh8MSsc3CYODotSFB-phCs_GqJHLa1TP_GAo8D_ubGdVVe=w640-h502


BAO pekee la Christian Bahera dakika ya limeipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu Kufuz Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 20 Costa Rica baadaye mwaka huu.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Tanzanite ingeweza kupata mabao zaidi kama igetumia vyema nafasi ilizopata.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TANZANITE YAENDA KUWEKA KAMBI KARATU.​

AVvXsEgnA_QgW3j0rXahe65GAbRfG5uJd35-yp75aAcF-CTzA_9vdT6Yvy3KAK34_xUhNixf00Nv06bK2OY3y4JuqQzUfoS_oq0acAJLtezsh97BkcouAGnr0V0b5at16WZPGZPvRgyfldQWu8LBqaKRduq4splYv2dfNZFXjrqa336fRI78wDjX-38EnVLK=w640-h480

BAADA ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia jana katika mchezo wa Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 20 baadaye mwaka huu nchini Costa Rica, kikosi cha Tanzanite kimeondoka leo Zanzibar kwenda Karatu kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano.
Tanzanite ambayo bao lake pekee lilifungwa na Christian Bahera Uwanja wa Amaan jana, imewkea katika katika hosteli za akademi ya Black Rhino mjini humo kujiandaa na mchezo wa marudiano ambao utafanyika Februari 4 Jijini Addis Ababa.
AVvXsEjTegVlqNkGF8zYJ5hds5Yy5VuQhnghTwxL3SqNC_IGOZO5DS8tvdfAh0W2mPbnrp0_qpSO4q_TVFt6BjZwU9f7yRd-RZ6Nzzk70YmSRiMSVKd_QZQepJ98024NCVyRgIFBT3gT51kr6yjXsr7AMQ6dIBMgn7ABkDwnqOm5Z4CW8JOHjFj__J08rZ8o=w640-h482
\
AVvXsEj2oDXKcLf4IBcelspwCZtgpibkEvGKXehLYcubCn3erIsIuYEHQOJuX1I-oiS-08ihZwEu74fCXlWlV0Wu_ljNU39F6CUWlpG9AvxtAxKI_wz3u9xlx5guI9YxVMpdPleZEuRJuzdqVb8IG029KxL2QJSzf2t8wr-YhhFlbyc1quZ3Hv0SC0MQdC9m=w640-h480
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TANZANITE YAIFUATA ETHIOPIA MECHI YA MARUDIANO.​

AVvXsEjPTMgn4N0-5vgvlsweMob2x7fBE1eqx0bk-eDHom34KNi8GbjdCsUg4YDRuYCd_QFJVF-6u0YwUfEQTihg-qJRtPmDT0Pp8va-9kMc5TpEO9CYoEoumyRAFpIESSWMCfUccskju_ub_KToO3y0SFCtYDSsrvskGBkSKiLPceJmHPrbOxDg847tTIPt=w512-h640

KIKOSI cha timu ya taifa za wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite kimeondoka leo jioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudano na wenyeji kufuzu Kombe la Dunia Ijumaa Jijini Addis Ababa.
Tanzanite ambayo iliweka kambi ya wiki moja akademi ya Black Rhino, Karatu mkoani Manyara - inahitaji sare katika mchezo huo kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Aman, Zanzibar.
Ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakutana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Ghana, ambao ni mtihani wa mwisho utakaotoa tiketi ya kwenda Costa Rica katika Fainali zitakazoanza Agosti 10 hadi 28, mwaka huu.

AVvXsEiQxzhQD0gy-OLng2BNkcxhirxQxc5Rb7uxlDfyquzjCjxrdiROdMUBsgSoF8s8nSZhlhltRI50XmNxQcp4LO5Jc0-KXTP8Z7G6xu4ggsO64W58tvv9qf0CweHUja1O4NXCPPjRp8aNmhtLQIk-RlfBF1XRD6IWNCRA4JqZ3FXK8vVgdOKcyZZIGlNO=w640-h480
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

TANZANITE YACHAPWA 2-0 NA ETHIOPIA ADDIS ABABA.​

AVvXsEgDATcSEMQ1TLvrWt9NziSCdkxjKn00_u69gYDWcy6tktHhtVFzSieBzVvTLE7zzy7iP_lYgWOuunDCq6pNGDj32mHUtgS9HpSaZYYinDVp2XcgxTiE01vkjEdywjv8bACe2tp__o3eKRf71jNMyIs_UMkaqZGiJSWPTNXkkOv4XbsjlpcYRyo_WA70=w640-h640

TIMU ya taifa za wasichana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania. Tanzanite imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Ethiopia katika mchezo wa marudano Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia jioni ya leo Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.
Kwa matokeo hayo, Tanzanite inatolewa kwa jumla ya kichapo cha 2-1 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Aman, Zanzibar.
Sasa Ethiopia itakutana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Ghana, ambao ni mtihani wa mwisho utakaotoa tiketi ya kwenda Costa Rica katika Fainali zitakazoanza Agosti 10 hadi 28, mwaka huu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA TANZANITE ADDIS.​

AVvXsEhfolar-4EaheWg1cVbS4N1-Vw62Ny0LPZfUZMMRkUXEJsaGklpeb2JQFzK3juMoJkfS7DENxC3f7Ol73P2iL5vf6kO5FvqOOm5RNj62wJx75-7X-3n8SLlKPgPmbmm_qLRMZrfdtGutWfGUi-HWo204Q4fffXSdsaqPTNV_rVVZtvQgJfGjafAWG1J=w640-h480

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Phillip Mpango amekutana na Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Dkt. Mpango amezungumza nao na kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ethiopia utakaochezwa leo saa 10 jioni kwenye uwanja wa Abebe Bikila.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TANZANIA U17 TAYARI KUIVAA BOTSWANA JUMAPILI KOMBE LA DUNIA​


WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 wakifanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Botswana Jumapili Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MABINTI WA TANZANIA WAWACHAPA BOTSWANA 7-0​

AVvXsEghJVDhSoa7NPFRE9uWpmiAls9GxaFEkcXZlSYqt8X0zObkYEnHyv6etNuCfYNwiiOVu2ujp69PhvcM98-mSPdwpVC_MH_osHmUcM2AvAHegYOjfhLz63z9jFB2s1ZVermm8zDucSQ4kx9sBGwkPYa5l_Igzabef3GVC0XqlTLX5lJt4xzZHwJ_tBJa=w640-h424

TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, imeitandika Botswana mabao 7-0 jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini India.
Mabao ya Tanzania U17 leo yamefungwa na Neema Paul na Clara Luvanga kila mmoja mawili na Aisha Juma matatu.
Timu hizo zitarudiana Machi 20 Uwanja wa Obed Itani Chilume Jijini Francistown na mshindi wa jumla atakutana na Burundi katika Raundi ya Tatu kuwania kwenda Raundi ya mwisho ya mchujo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RAIS SAMIA AWACHANGIA SH MILIONI 15 TWIGA STARS​


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ameahidi kuichangia timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kiasi Sh. Milioni 15.
Rais Samia alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwa simu na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba kwenye tamasha la harambee ya kuchangia Twiga Stars lililopewa jina, Orange Concect.
Kwa upande wake, Waziri Nchemba ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kutoa udhamini kwenye timu za wanawake ili ziweze kuendelea kufanya vizuri.
Nchemba amesema Mheshimiwa Rais amefanya mambo makubwa siyo tu kwenye sekta ya Michezo bali katika sekta mbalimbali.


Ametaja baadhi ya mambo makubwa ambayo Serikali imefanya kuwa ni maboresho makubwa kwenye huduma za jamii.
Pia amesema Mhe. Rais alivyoingia madarakani alielekeza watoa huduma walipwe madeni na maisha yao yameboreka.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

WAZIRI WA MICHEZO AWATEMBELEA WASICHANA U17​

AVvXsEjkSr2Tghl_66y9gqmSrrlCO-IIxwwFu-1NngMrUSnMf7OTqC9BZMa7V73KhRy09IxwAIoSdeZeMlAzjVUZgnBa6pQ9trsz74b01vYPdV7ePL0i5glKWEYktZirg-GhJQWx4SOgqpitV-liq7Bgl1QwJ5Jo-GeMiW5GSAjCGIh-rewVI2vfqvWQhJf0=w640-h478

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 iliyoweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Botswana Machi 20, 2022.
Mabinti wa Tanzania U17 walishinda 7-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita na wakivuka hatua hii watakutana na Burundi katika Raundi ya Tatu kuwania kwenda Raundi ya mwisho ya mchujo.
AVvXsEgf3IGbCuy-WDQWqVdCYXeEi2OOIA-qanPnA6DIfLMnVZ_bVr3w_EgPPprKRqGjPTDJ1JtlVB44vSBdtp6VxSA7NBTFzFrUTWRbcPfF0sazoQJw5sbwI-SC6x_zVAxx-PuZ-x1mmnT_o5ZcE-y2CjWPgA4dhR_3NlBUVrqSueOOWlS3cY1-5MStGhcV=w640-h478
AVvXsEgP1b0bh9sEw5113H4K59D5n7PqH57hptySOK9Jcbz6zNFjrg8cdodzSlTheKuZFl2II-EAe-oWk0ADJCYNKJ20c33ZmSKcvulR28rr4V4fF3yGMNZw6zNAYwO_LrvlHSNmUs0fYzdX0hzLBoIBogl1ag3fPVT9Xj875HNrPJub1WUwLlYTdTn3QRiI=w640-h478
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TANZANIA YASONGA MBELE KOMBE LA DUNIA WASICHANA U17​

EFF9C7E5-81A4-4F26-BE2B-7FA3D19C629C.jpeg

TIMU ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, leo imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Botswana leo Uwanja wa Francistown mjini Francistown.
Mabao ya Tanzania yamefungwa na Neema Kinega dakika ya 28 na Clara Luvanga matatu dakika za 62, 63 na 81 na kwa matokeo hayo inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 11-0 kufuatia kuwachapa Botswana 8-0 kwenye mechi ya kwanza Zanzibar.
Sasa Tanzania itamenyana na Burundi kuwania kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India baadaye mwaka huu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MABINTI WAREJEA FURAHA YA USHINDI​

D44B8FB1-8240-4B7E-8786-C6BA7D131675.jpeg

TIMU ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 imerejea jana usiku kutoka Botswana baada ya Jumapili kufanikiwa kwenda Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji.
Tanzania ile songa mbele kwa ushindi wa jumla wa 11-0, kufuatia mechi ya kwanza kushinda 8-0 Zanzibar.
Na sasa itamenyana na Burundi kuwania kuingia hatua ya mwisho ya mchujo ambako watamenyana na mshindi katinya Cameroon na Zambia, mtihani ambao wakiuvuka watakwenda India 2022.
0B83FD35-9C81-4167-8C9C-B9DBFDDDED35.jpeg

DD5D8F0E-4946-4141-A3F1-62531E917CDF.jpeg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SERENGETI GIRLS YATANGULIZA MGUU MMOJA KOMBE LA DUNIA​


TANZANIA imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Cameroon katika mchezo wa kwanza Raundi ya mwisho kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17, baadaye mwaka huu nchini India.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana William dakika ya tatu na Clara Luvanga mengine yote matatu dakika za 29, 63 na 71 huku la wenyeji likifungwa na Mona Lamine dakika ya 26.
Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Dar es Salaam, Serengeti Girls ikihitaji kuulinda ushindi wake ili kwenda India.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

CAMEROON HAWAKUAMINI ALIYEPIGA HAT TRICK NI BINTI​


MAAFISA wa Cameroon jana wamedaiwa kumkagua jinsia yake mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga ili kujiridhisha ni mwanamke kabla ya mchezo wa kwanza Raundi ya mwisho kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Serengeti Girls ilishinda 4-1, huku Clara anayechezea Yanga Princess akipiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za 29, 63 na 71 baada ya Diana William kufunga la kwanza dakika ya tatu, wakati na la wenyeji likifungwa na Mona Lamine dakika ya 26.
Pongezi kwa maafisa wa Tanzania walioambatana na timu hiyo kwa kumjenga kisaikolojia Clara pamoja na udhalilishaji huo aliofanyiwa, adha kama ambayo aliwahi kuipata mwanariadha wa Afrika Kusini, Caster Semenya ambaye baadhi wa watu walikuwa wanamtazama Caster kama mwanaume, sio mwanamke.
Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Zanzibar, Serengeti Girls ikihitaji kuulinda ushindi wake ili kwenda India.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SERENGETI GIRLS WAPEWA HESHIMA YA KIPEKEE BUNGENI​



TIMU ya taifa ya wanawake ya soka chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza kupewa heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuingia na kukaa kwenye viti vya mawaziri ndani ya bunge baada ya kufuzu kuingia mashindano ya dunia ikiwa ni heshima ya mashujaa wa Taifa kwa kazi kubwa iliyoifanya ambapo kesho ni zamu ya Timu ya soka ya Taifa ya Walemavu ya (Tembo Warriors) ambayo pia imefuzu mashindano ya dunia ya soka kwa walemavu.
Akiongea mara baada ya kuketi eneo hilo rasmi la mawaziri, Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema ushindi huo unatokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuiwezesha timu hiyo katika kipindi chote cha maandalizi wa mashindano hayo.
“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha, kututia moyo na kutufuatilia kwa karibu sana katika kipindi chote” amefafanua Mhe. Mchengerwa.





Aidha, amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuisaidia timu hiyo ili iweze kwenda na kushinda kwenye mashindano hayo hatimaye kurejesha kombe hilo la dunia na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kuwatia moyo na kuwasaidia ili washinde.
Akizungumzia jinsi timu ilivyopambana hadi kufika hapo amesema kuwa timu ilianza kuchabanga Botswana magoli 11-0, ikaitandika Burundi jumla ya magoli 6-1, na ikamalizia na kuibamiza timu ya Cameroon jumla ya magoli 5-1.
Kwa upande wa Warriors amesema iliishindilia Cameroon mabao 5-0, kabla ya kuikandamiza Senegal goli 1-0 na kuichakaza Morroco magoli 2-0.
Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kufanya mapinduzi makubwa katika sekta za michezo na Sanaa ili kuipeleka Tanzania kimataifa ambapo amefafanua kuwa kuanzia Februari mwaka huu timu zote za taifa zinazoshiriki kwenya mashindano ya kimataifa zimewekwa kambini na zinagharimiwa na Serikali.
Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo Noela Luhala alipewa heshima ya kuzungumza mbele ya Bunge tukufu ambapo ameishukuru Serikali na Bunge kwa mchango iliyowapa. @serengetigirlstz
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

FIFA YAIPONGEZA TANZANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA​




SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeipongeza Tanzania kwa kufanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri was miaka 17 zitakazofanyika India baadaye mwaka huu.

 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

WAZIRI AWAPONGEZA MABINTI KWA KUTWAA UBINGWA WA KRIKETI RWANDA​



WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwa Timu ya Tanzania ya Wanawake ya Kriketi kwa kutwaa Ubingwa Juni 18, 2022 kwenye mashindano ya Kwibuka Cup nchini Rwanda, yaliyoshirikisha nchi nane( Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana , Nigeria, Brazil na Ujerumani) bila kufungwa na timu yoyote.
Aidha, amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa anaoutoa katika michezo.
Amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha michezo kwa kuweka mikakati kabambe chini ya uongozi wa Samia imeleta matokeo chanya kwenye sekta za michezo na sanaa hapa nchini.
Amesema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi iliyosomwa bungeni hivi karibuni imeonesha kuwa sanaa na burudani zimechangia kwa asilimia 19.4 katika kipindi cha mwaka 2021 na kuziacha kwa mbali sekta mbalimbali.
Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi badala mazoe ya kuifanya michezo kama kitu cha burudani pekee.
Aidha, amesema Serikali tayari inazigharimia timu zote za taifa zinazojiandaa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuziweka kambini kuanzia mwanzo wa mwaka huu.
Hivi karibuni Mhe. Mchengerwa amekaririwa vyombo vya habari akisisitiza kuwa michezo na sanaa ni uchumi hivyo wanamichezo na wasanii wanapaswa kutambua kuwa vipaji walivyonavyo ni mtaji wa maisha yao.
Ujumbe wa Klabu ya Southampton uliokutana na Mhe. Waziri Mchengerwa na kufanya mazungumzo ya kuinua michezo ulioongozwa na Mkuu wa Idara ya Biashara ya klabu hiyo David Thomas pia ulimpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye michezo na kumzawadia jezi ambayo ilipokelewa kwa niaba yake na Mhe. Mchengerwa.