Technology inayotumika World cup ya Qatar haijawahi kutumika kokote Duniani. Mipira ya world cup inachajiwa ! UNAJUA ?

Brenda

Mgeni
Oct 31, 2022
489
403
5
Dar es salaam
Mipira inayotumiwa kwenye kombe Dunia Qatar πŸ‡ΆπŸ‡¦ 2022 iliyobuniwa na kampuni ya ADIDAS, imetengenezwa ikiwa na bettery ndogo ndani yake ambayo huisha charge baada ya saa sita.. Huisha charge baada ya saa (6) iwapo inatumika na siku kumi na nane (18) ikiwa haitumiki.

SENSOR yake ambayo ina uzito wa 14 grams hutumika ku-support technology ya Camera mbalimbali zilizofungwa kwenye pitch ambazo huwasaidia waamuzi kwenye matukio tata na OFFSIDE.

Kila mpira unapopigwa kwa mguu au kichwa nk.. SYSTEM huchora mistari zaidi ya 500 kwa sekunde moja ili kubainisha kama kuna Offside, Faulo na vitu kama hivyo..

.... Data hutumwa immediately kutoka kwenye SENSOR kwenda kwenye LOCAL POSITIONING SYSTEM (LPS), system ambayo inajumuisha setup ya network za antenna zote ambazo ziko installed kuzunguka eneo lote la kuchezea na Data huhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya muda huo na matumizi ya baadae.

Iwapo mpira utapigwa nje ya eneo lililofungwa System hiyo na mpira mpya ukarushwa au kupigwa ndani ya pitch ku-replace mpira uliotoka, KINEXON 's BACKEND SYSTEM automatically hu-switch kutoka ule mpira uliotoka kwenda kwenye INPUT DATA za mpira ulioingia bila kuhitaji msaada wa binadamu...... Chukua hiyo .... ✍️