Tetesi Zote Za Usajili Bongo

Mshua

Mgeni
May 27, 2024
34
24
5
UONGOZI wa Singida Black Stars umeanza kufuatilia kwa karibu saini ya beki wa kulia wa KMC, Abdallah Said Ali 'Lanso'.
Lanso alitua KMC katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Mlandege Zanzibar na kusaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele kinachomruhusu kuondoka akipata timu na Singida inataka kukitumia.

NYOTA wa Dodoma Jiji, Abubakar Ngalema ameanza kuwindwa na klabu kadhaa, huku Kagera Sugar na Pamba Jiji zikitajwa kuwa karibu kunasa saini yake.
Beki huyo wa kushoto, mkataba wake na Dodoma umemalizika na hayupo tayari kuendelea na kikosi hicho baada ya kukitumikia kwa miaka minne.

SINGIDA Black Stars, imeanza mazungumzo ya kumpata aliyekuwa nyota wa KMC, George Makang'a ambaye yupo huru kwa sasa.
Makang'a aliyejiunga na KMC mwaka 2022 akitokea Mtibwa Sugar amemaliza mkataba huku kukiwa bado hakuna maelewano mazuri ya kuongeza mwingine, hivyo Singida imeanza mazungumzo kumnasa.

BAADA ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, Pamba Jiji inadaiwa imeanza mbio za kumnasa beki wa kati wa Mashujaa, Samson Madeleke aliyemaliza mkataba na timu hiyo iliyonusurika kushuka daraja.
Madeleke aliyejiunga na Mashujaa katika dirisha dogo lililopita akitokea Mbeya City inaelezwa ameanza mazungumzo na Pamba iliyorejea Ligi Kuu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 20 tangu iliposhuka 2001.

UKIACHANA na Simba na Yanga kuitaka saini ya winga machachari wa JKT Queens, Winifrida Gerald, timu ya Amani Queens nayo imeingia katika vita hiyo.
Amani inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) ipo katika mazungumzo na winga huyo anayemaliza mkataba JKT, aliyojiunga nayo msimu uliopita akitoka Fountain Gate Princess na kuifungia mabao 11.

BAADA ya kunusurika kushuka daraja, Alliance Girls inaendelea kuimarisha kikosi ikielezwa ipo mbioni kuwasajili wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Kenya.
Inadaiwa Alliance ipo katika hatua nzuri ya kunasa mabeki wawili, Lupemeba Bilonda anayekipiga Thika Queens na Centrine Wasike wa Bungoma Queens.

KLABU ya KMC inaelezwa haitokuwa na mchezaji wa timu hiyo msimu ujao, Sadala Lipangile baada ya kuichezea kwa takribani miaka saba.
Sadala anayemudu kucheza eneo la beki wa kati na mshambuliaji, alijiunga na KMC mwaka 2017 akitokea Mbao FC ya jijini Mwanza, huku ikielezwa tayari klabu mbalimbali zimeanza kuiwinda saini yake zikiwemo KenGold, Pamba Jiji na Mashujaa.