Tuangazie Match ya Arsenal vs Man United leo saa 19:30

McRay

Mgeni
Nov 4, 2022
185
131
5
Mechi ya Arsenal vs Man utd leo ni moja ya mechi ngumu sana kwa washabiki wa timu hizo lakini mechi nzuri kwa wasio washabiki wa hizi timu.

Arteta vs Ten Hag
Hii ni ligi inayokuja kuteka EPL soon, makocha wanaoonyesha kurejesha makali ya hizi timu na kuwapa moyo washabiki wao kuwa siku za ushindani wa mpira kwa timu zao unarejea.

Makocha hawa wawili wametokea kuzirejesha timu zao makali yaliyopotea ndani ya muda ambao wapenzi wa mpira hawakutaraji kuwa mapema hivi.
Arsenal wakianza na malengo ya kurudi top 4 mwanzoni lakini kwa sasa wao ndo wameshikilia ufunguo wa ubingwa wa ligi, malengo yanaelekea kubadilika ama yameshabadilika.

Ten Hag vile vile mafanikio makubwa msimu huu ilikuwa kuingia top 4 , lakini kutokana na muendelezo wa kiwango cha timu na wao wametokea kuwa wapinzani wa ubingwa huenda kutokana na wapinzani waliotarajiwa kabla ya msimu kuanza.

Silaha ya makocha hawa wawili ni mbinu katika mchezo husika wanaokutana nao, nguvu nyingine ni namna wanavyowahamasisha wachezaji wao kucheza kitimu na kujitoa kila jasho na hatimae kuonekana ni timu ngumu kufungika.

Timu zote mbili zina sifa za kufanana.
1. Timu zote zina washambuliaji vijana wenye uchu wa kutengeneza nafasi na kufunga.
2. Timu zote zina viungo mahili wa kutengeneza nafasi, kujilinda na kufunga.
3.timu zote zina magolikipa walio katika uwezo binafsi wa kubeba timu katika wakati mgumu.
4.timu zote ni waumini wa mfumo wa 4-2-1-3 , 4-3-3, -4-1-2-3 kutegemea na mpinzani.

Kukosekana kwa Casemiro katika eneo la kiungo kwa utd ni pigo kubwa kwa timu, lakini pia kutizama mpambano wa Partey vs Casemiro lilikuwa jambo zuri kwa shabiki wa soka kutizama. Lakini katika mpira kukosekana kwa Mchezaji muhimu kunaweza kuzibwa na Mchezaji mbadala ama mfumo wa timu kubadilika au hata set up ya timu pia kubadilika.

Sare inaweza kuwa matokeo fare kutokana na form ya hizi timu kwa sasa. Ukizingatia mechi ya kesho inaweza kuwa ya tahadhari kwa kila upande kutotaka kupoteza au kila mmoja kutaka kushinda.
E9A1BC63-3AFE-4DB5-9584-B15B94B27702.jpeg