Kocha Mkuu wa klabu ya Sheriff Tiraspol ya Moldova
Yuriy Vernydub (56) raia wa Ukraine
amerejea kwao kwaajili ya kuipambania nchi yake inayoshambuliwa na Urusi.
Yuriy ambaye aliwahi kupita jeshini kwa kipindi cha miaka miwili wakati akiwa kijana, amesema aliposikia kuwa Russia wamewavamia akaiambia familia yake pamoja na wajukuu zake kuwa yupo tayari kurejea na kupambania nchi yake.
" Mke wangu, Watoto wangu pamoja na wajukuu wamenishauri mara nyingi sana nisifanye hivyo lakini nimewaambia siwezi lazima niipambanie nchi, wananijua vizuri, nikiamua jambo huwa sibadiliki"
"Nimewaambia kama wao watahama nchi sawa ila mimi na mke wangu tutabaki hapa kwaajili ya nchi yetu"
"Sitaki kusema nilikuwa nafasi gani jeshini lakini wajue kuwa najua namna ya kutumia silaha na mbinu zote za kivita, nipo hapa nitapambania Taifa langu kwa nguvu zote"
"Najua Vijana wengi wamekimbia nchi, nawashauri warudi tuungane kwa pamoja tupambanie nchi yetu, hakuna msaada mwingine bila sisi wenyewe kujipambania" alisema Yuriy
Ikumbukwe kocha huyo ametengeneza historia kubwa kwa kuiiongoza Sheriff Tiraspol kushinda mabao 2-1 katika mchezo Ligi ya Mabingwa dhidi ya wababe wa michuano hiyo Real Madrid katika hatua ya makundi.
Sasa ni mwanajeshi anayepigana dhidi ya uvamizi wa Warusi katika nchi yake