Unakubaliana Na Kauli Hii Ya Kocha Mkuu Wa TAIFA STARS Kuhusu Makundi Ya AFCON 2025? Ukipata Nafasi Ya Kumshauri Ungemwambia Kipi?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
501
662
125
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Seleman 'Morocco' ametoa mtazamo wake na namna watakavyokiandaa kikosi kwenda kushindana na sio kushiriki pekee katika michuano itakayoanza Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026 nchini Morocco, Taifa Stars imepangwa kundi C na timu za Nigeria, Tunisia na Uganda.

"Kwangu mimi sijaona kundi rahisi likiwemo hili letu, yote ni magumu, Tanzania sio wanyonge, nipo hapa Morocco na makocha mbalimbali ukijitambulisha unatoka Tanzania wanaheshimu sana na hata baada ya droo unaona washindani wetu wanatafakari kwa kina," amesema Morocco na kuongeza.

"Tanzania imeshatoka kwenye enzi za unyonge, tunatakiwa tujiamini kama Taifa kwamba tunaweza kufanya kikubwa, miaka ya nyuma tulikuwa tunakuja kama wasindikizaji, fainali zilizopita tukafanikiwa kupata pointi kwenye makundi, safari hii tunataka kuja kushindana kutafuta nafasi mbili za juu kwenda mbali."

Stars inakwenda kushiriki Afcon 2025 kwa mara ya nne baada ya kufanya hivyo mwaka 1980 (Nigeria), 2019 (Misri) na 2023 (Ivory Coast).
Katika Afcon ya 2019, ndiyo pekee ambayo Stars iliondoka bila ya pointi lakini 1980 ilipata pointi moja na 2023 pointi 2 ingawa mara zote imeishia hatua ya makundi.
 
  • Like
Reactions: Giant

stuadydigason

Mpiga Chabo
Aug 1, 2024
13
0
0
Tanga
Morroco ni kocha mzuri na kocha mzalendo mpenda inchin yake
Jambo la kuzingatia ni kupanga kikosi kulingana na mpinzani wake katika mechi
Licha ya bado kuhitajika nguvu na akili nyingi katika kufikia lengo
#@Taifastar inakikosi kizuri #
Mwalim moroco aende na mbinu kadha kuimairsha kikosi na kuamini kwamba taifa lina hitaji kupeperushwa kwa bendera yetu💪💪
 
osi gadi

Mpiga Chabo
Jan 28, 2025
1
0
0
Kocha yupo sahihi kabisa,,,kwa sasa sisi watanzania tunaenda afcon kupamabana na sio tu wasindikizaji...Mungu ibariki Tanzania.
 
Vej Jr.

Mpiga Chabo
Sep 8, 2024
2
0
0
Ya Mungu ni mengi,,, nani anajua kama Guinea angetoka,,!? hakuna
kiuhalisia kundi ni gumu sana ila inshu kubwa ni kwenye maandalizi, wachezaji watakaoitwa wawe bora, kila mchezo kocha awe na mbinu za kutosha kuhakikisha tunachokipambania kama Taifa kinapatikana lakini zaidi wachezaji wawe na utayari (morali) kutoka ndani kuona haja ya kupambana tunaweza kufika nchi ya ahadi kwa ushindi..!!
 
Mnakane Sr.

Mgeni
Oct 7, 2024
5
1
5
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Seleman 'Morocco' ametoa mtazamo wake na namna watakavyokiandaa kikosi kwenda kushindana na sio kushiriki pekee katika michuano itakayoanza Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026 nchini Morocco, Taifa Stars imepangwa kundi C na timu za Nigeria, Tunisia na Uganda.

"Kwangu mimi sijaona kundi rahisi likiwemo hili letu, yote ni magumu, Tanzania sio wanyonge, nipo hapa Morocco na makocha mbalimbali ukijitambulisha unatoka Tanzania wanaheshimu sana na hata baada ya droo unaona washindani wetu wanatafakari kwa kina," amesema Morocco na kuongeza.

"Tanzania imeshatoka kwenye enzi za unyonge, tunatakiwa tujiamini kama Taifa kwamba tunaweza kufanya kikubwa, miaka ya nyuma tulikuwa tunakuja kama wasindikizaji, fainali zilizopita tukafanikiwa kupata pointi kwenye makundi, safari hii tunataka kuja kushindana kutafuta nafasi mbili za juu kwenda mbali."

Stars inakwenda kushiriki Afcon 2025 kwa mara ya nne baada ya kufanya hivyo mwaka 1980 (Nigeria), 2019 (Misri) na 2023 (Ivory Coast).
Katika Afcon ya 2019, ndiyo pekee ambayo Stars iliondoka bila ya pointi lakini 1980 ilipata pointi moja na 2023 pointi 2 ingawa mara zote imeishia hatua ya makundi.
Naungana nae,
Siyo Kinyonge tena aiseee ingawa tunatakiwa kukaza
 
Butali

Mpiga Chabo
Jan 28, 2025
2
0
0
Tunamuamin coch hemed moroko Kwan yey ameweza kuchukua ubingwa wa Zanzibar heros mbele ya bukina faso
Hakik huu Ndo mwak wetu taifa stars kuvuka makundi na kusong mbele
 
SHAMIL

Mpiga Chabo
Jan 29, 2025
2
0
0
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Seleman 'Morocco' ametoa mtazamo wake na namna watakavyokiandaa kikosi kwenda kushindana na sio kushiriki pekee katika michuano itakayoanza Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026 nchini Morocco, Taifa Stars imepangwa kundi C na timu za Nigeria, Tunisia na Uganda.

"Kwangu mimi sijaona kundi rahisi likiwemo hili letu, yote ni magumu, Tanzania sio wanyonge, nipo hapa Morocco na makocha mbalimbali ukijitambulisha unatoka Tanzania wanaheshimu sana na hata baada ya droo unaona washindani wetu wanatafakari kwa kina," amesema Morocco na kuongeza.

"Tanzania imeshatoka kwenye enzi za unyonge, tunatakiwa tujiamini kama Taifa kwamba tunaweza kufanya kikubwa, miaka ya nyuma tulikuwa tunakuja kama wasindikizaji, fainali zilizopita tukafanikiwa kupata pointi kwenye makundi, safari hii tunataka kuja kushindana kutafuta nafasi mbili za juu kwenda mbali."

Stars inakwenda kushiriki Afcon 2025 kwa mara ya nne baada ya kufanya hivyo mwaka 1980 (Nigeria), 2019 (Misri) na 2023 (Ivory Coast).
Katika Afcon ya 2019, ndiyo pekee ambayo Stars iliondoka bila ya pointi lakini 1980 ilipata pointi moja na 2023 pointi 2 ingawa mara zote imeishia hatua ya makundi.
Hilo ni suala la muda tu tukambanie nchi yetu