Upi mtazamo wako katika vita ya Simba, GSM na TFF?

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
ISHU ya mkataba wa GSM na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imebadilika baada ya jana Simba kugomea mkutano wa maandalizi sababu kubwa ikitajwa ni kuwemo na mabango ya mdhamini mwenza huyo wa Ligi Kuu Bara.

Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa TFF uliopo Karume huku wawakilishi wa Simba nao walifika wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Ally Shatry ambaye alisikika akitamka kuwa “Toeni bango kwanza”. Badae Simba waliondoka zao. Kauli hiyo ya ilikuja baada ya Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo kuwataka Simba waingie ndani kwani muda wa mkutano ulikuwa umefika na tayari kocha wa Yanga, Nassredine Nabi ndiye aliyeanza kuzungumza na kumaliza.

Baada ya Simba kugoma kuingia Ndimbo aliwaruhusu wadhamini wakuu wa Ligi, NBC kuingia. Simba walishaandika kuomba ufafanuzi juu ya udhamini wa TFF na GSM. Ofisa Habari, Karim Boimanda alisema; “Huo mkataba baada ya kuuona ulichukuliwa vipande vinavyotuhusu sisi kama bodi na kuzipatia klabu, hivyo kinachoendelea kitamalizwa na kanuni,”. Simba wanasisitiza kwamba wanataka kujua undani wa mkataba huo na kila kitu kilichopo kinawanufaishaje wao.

Je mtazamo wako katika vita hii ni upi?

simba-tff-pic.jpg
 
  • Like
Reactions: JimNicklaus