USAJILI.

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
BREAKING: Klabu ya Fc Barcelona imekamilisha usajili wa winga wa Wolves Adama Traore
🇪🇸
kwa mkopo wa miezi sita wenye chaguo la kumsajili moja kwa moja kwa dau la €30m
Adama atasaini mkataba wa miaka mitano mara baada ya kumalizika kwa muda wake wa Mkopo kama Barcelona watataka kumsajili kwa usajili wa kudumu
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanacheza kandakanda na watu wanasimama
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Frank Lampard anatarajiwa kutangazwa na kusaini mkataba wa kuwa kocha Mkuu wa Everton hii leo. Tayari ameanza kushughulikia usajili wa Donny van de Beek kwa mkopo akitokea Manchester United. Chanzo: Fabrizio Romano.
Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Kwa mujibu wa Daily Mail, Ousmane Dembélé anakaribia kujiunga na timu mojawapo ya Premier League! Klabu mbili zimeonyesha nia ya kulipa kiasi cha €20M ili kuipata saini yake. Barça hawana mpango wa kubaki nae licha ya mchezaji huyo kuomba asalie.
Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Pierre Emerick Aubameyang ametua jijini Barcelona
🇪🇸
kwaajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Fc Barcelona kwa mkopo.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na miwani ya jua
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa Joe Edwards amejiunga na Everton kama kocha Msaidizi chini ya Frank Lampard.
Marafiki wamekutana tena kazini.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Klabu ya Fc Barcelona imekamilisha usajili wa Pierre Emerick Aubameyang akitokea Arsenal kwa usajili wa bure.
Arsenal hawakutaka kiasi chochote cha pesa kutoka Barcelona, walichotaka ni Aubameyang kuondoka.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
OFFICIAL: Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Mali
🇲🇱
Ibrahima Koné (22) amejiunga na
🇫🇷
Lorient akitokea Sarsporg 08 kwa ada ya €3m.
Konè ambaye amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michuano ya AFCON mwaka huu, ataitumikia Lorient hadi mwaka 2026.
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na ndani
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Kocha wa Fc Barcelona Xavi Hernandez ameiomba klabu hiyo imsajili mlinzi wa kati wa Sevilla Jules Koundé ifikapo mwishoni mwa msimu huu
Kwa mujibu wa SPORT, Fc Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji hatari wa kati pamoja na kuboresha eneo la ulinzi mara baada ya kumalizika kwa msimu huu
Wanaotajwa ni:
➡️
Erling Haaland (Dortmund)
➡️
Tagliafico (Ajax)
➡️
Jules Kounde (Sevilla)
Barcelona
🇪🇸
wameamua kutengeneza timu sasa.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi yanayosema 'Liga'

 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Real Madrid imepanga kumpa ofa ya mshahara wa €25M (Bilioni 65.6
🇹🇿
) kwa mwaka mshambuliaji wa PSG
🇫🇷
Kylian Mbappe atakapojiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu
Mshahara huo ni baada ya kulipa kodi
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Klabu ya Chelsea imepanga kutumia kiasi cha €200m (Bilioni 525
🇹🇿
) kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji watatu ifikapo mwishoni mwa msimu huu:
🇫🇷
Jules Koundé
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Declan Rice
🇫🇷
Aurélien Tchouameni
(Source: Telegraph)
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Sura mpya za maana kwenye rada za EPL.​

Sajili PIC

LONDON, ENGLAND. MASHABIKI wa Ligi Kuu England wamekuwa na bahati ya kushuhudia mastaa wa maana kwenye ligi hiyo wanaotoka ligi za nje na kwenda kukipiga humo katika miongo michache ya hivi karibuni.
Na hilo linakwenda kutokea tena kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo kuna wakali matata kabisa wanaotamba kweye ligi za nje watatua Ligi Kuu England kutokana na klabu kibao kwenye ligi hiyo kuhusishwa na mpango wa kuwasajili.
-Erling Haaland. Hakuna ishu yoyote inayohusu tetesi za usajili zikaacha kuhusiana jina la straika huyo wa Borussia Dortmund. Staa huyo wa Norway amekuwa kwenye rada za timu nyingi ikiwamo Real Madrid na Barcelona - lakini timu za Ligi Kuu England zimekuwa na jeuri ya pesa ambazo zinawapa nafasi kubwa ya kumsajili Haaland, ikiwamo Manchester City, Manchester United, Chelsea na Liverpool ambazo zimekuwa zikihitaji saini ya mchezaji huyo atakayepatikana kwa ada isiyozidi Pauni 68 milioni mwisho wa msimu.
-Rafael Leao. Staa huyo wa AC Milan amekuwa akizivutia klabu nyingi sana za Ligi Kuu England msimu huu. Mbrazili huyo amefunga mabao 10 kutoka wingi ya kushoto huko Italia na Arsenal na Newcastle United wanapambana kuwania saini yake.
-Ronald Araujo. Man United na Liverpool imekuwa ikimfuatilia kwa karibu staa wa Barcelona, Ronald Araujo. Kocha Xavi anahitaji kubaki na beki huyo wa Uruguay hadi mwisho wa mkataba wake mwaka 2023, lakini bado hajakubaliana juu ya dili jipya na hilo linafanya klabu za Ligi Kuu England zimeanza kumfukuzia wakihitaji saini yake.
-Jules Kounde. Chelsea imeonyesha dhamira ya dhati kabisa ya kunasa saini ya beki wa Sevilla, Jules Kounde na bila ya shaka dili lake linaweza kukamilishwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi. Baada ya kumkosa kwenye dirisha lililopita, kocha Thomas Tuchel atafanya kila analoweza kunasa saini ya beki huyo kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
-Ousmane Dembele. Staa wa Barcelona, Ousmane Dembele anajiandaa kuachana na miamba hiyo ya Nou Camp na mara kwa mara amekuwa akihusishwa na klabu za Ligi Kuu England. Chelsea na Arsenal zimekuwa zikihusishwa na huduma yake na huenda mwisho wa msimu akatua EPL.
-Alexander Isak. Arsenal wanahitaji straika mpya na kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na mkali huyo anayekipiga Real Sociedad. Arsenal ilishindwa kunasa saini yake kwenye dirisha la Januari, hivyo itarudi kumsajili mwishoni mwa msimu huu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Conte: Nyota Tuliowasajili Januari Hamna Kitu​

Tottenham-Antonio-Conte-F365.jpg

KOCHA Antonio Conte amedai kuwa sera ya usajili ya Tottenham inadhoofisha kikosi, huku akiweka wazi kuwa wachezaji waliowasajili wakati wa dirisha la Januari wamekwenda kukiharibu zaidi kikosi chao badala ya kukiboresha.
Muitaliano huyo amedai kuwa timu yake sasa ina nafasi ya asilimia moja tu kumaliza top 4 katika Premier, Tottenham wanaivaa Man City leo Jumamosi ugenini wakitoka kupoteza mechi tatu mfululizo za Premier.
Katika usajili wa Januari, Spurs waliwaongeza viungo Dejan Kulusevski na Rodrigo Bentancur kutoka Juventus, huku Tanguy Ndombele, Bryan Gil, Dele Alli na Giovani Lo Celso wakiondoka “Badala ya kukiboresha kikosi, tumekidhoofisha,” alisema.
“Bentancur na Kulusevski ni wazuri kwa Tottenham siku zijazo, kwa sababu Tottenham wanatafuta wachezaji makinda, wanaweza kukua na kuendelea, siyo wachezaji walio tayari. Hili ni tatizo. Nimegundua sasa kwamba haya ndiyo maono ya klabu.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Joao Felix Anukia Arsenal​

felix.jpg

ARSENAL imetajwa kumuwania saini ya nyota wa Atletico Madrid, Joao Felix na kocha Mikel Arteta akitajwa kuwa na mpango naye Felix alijiunga na Atletico Madrid mwaka 2019 kwa pauni 113m kutoka Benfica ameshindwa kutamba kikosini hapo.
Inaelezwa kuwa majira ya joto mwaka huu kuna uwezekanao mkubwa kwa Felix kuondoka kikosini hapo na Atletico wakamsajili Concalo Guedes wa Valencia kama mbadala wake.
Ripoti zinaeleza kuwa Arsenal tayari wameanza kumfuatilia kwa ukaribu Mreno huyo hasa baada ya kumkosa Dusan Vlahhovic, Januari mwaka huu, Felix bado ana mkataba wa miaka minne na Atletico na kipengele cha kutaka kumuachia ni kiasi cha pauni 219m.
Imeelezwa kuwa Arteta anataka kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji licha ya Felix hivi karibuni kiwango chake kuonekana kusuasusa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Man City kulainisha dili la Kane Man United​

Kane PIC

MANCHESTER ENGLAND. MANCHESTER United ikifanikiwa kunasa huduma ya kocha Mauricio Pochettino, watatoboa kwenye mbio zao za kumsajili straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Kocha huyo wa Paris Saint-Germain, Pochettino amekuwa akitajwa kuwekwa kwenye orodha ya kwanza kwa makocha wanaosakwa huko Old Trafford kwenda kuchukua mikoba ya Ralf Rangnick, huku mabosi wengine wanaosakwa ni Erik ten Hag na Luis Enrique.
Harry Kane anaelezwa kwamba atamfuata Pochettino endapo kama atatua Old Trafford na hilo litasaidiwa zaidi na Manchester City kama watafanikiwa kunasa saini ya Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund.
Man City walihitaji saini ya Kane kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana, lakini walishindwa kuafikiana bei na Spurs, ambapo bosi wa timu hiyo, Daniel Levy alihitaji alipwe Pauni 160 milioni.
Kwa sasa kocha Pep Guardiola amehamishia nguvu kwa Haaland, jambo litakalowafanya Man United kuwa kwenye vita ya peke yao katika kufukuzia huduma ya Kane.
Man City wao wameshamsajili straika wa Kiargentina, Julian Alvarez, lakini imembakiza huko River Plate, hivyo kwenye dirisha lijalo hawatahitaji kutumia pesa nyingi kumsajili mshambuliaji na badala yake watamchukua Haaland, ambaye anaelezwa kwamba atapatikana kwa ada ya Pauni 64 milioni pekee kwa mujibu wa kipengele kilichochomekwa kwenye mkataba wake. Kane, ambaye amefunga mabao 24 kwa klabu na nchi yake msimu huu, bado ana mkataba mrefu huko Spurs hadi majira ya kiangazi 2024.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Messi anukia Marekani, Beckham asimamia shoo​

messi pic

INTER Miami imepanga kumshawishi staa wa Paris St-Germain na Argentina, Lionel Messi, 34, atue kikosini kwao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa staa huyo ataamua kuondoka kwenye timu yake.
Mkataba wa sasa wa Messi unatarajiwa kumalizika 2023 na amekuwa akitamani kucheza Ligi Kuu ya Marekani kabla ya kustaafu.
Kabla ya kutua PSG akitokea Barcelona, supastaa huyu alikuwa na asilimia kubwa kujiunga na Manchester City kwa sababu ilimhakikishia nafasi ya kucheza Marekani mara baada ya kumalizika kwa mkataba.
Inaelezwa kuwa Messi ameshaanza kujiandaa na maisha ya nchini humo kwani tayari ameshanunua nyumba.
Asilimia za Messi kujiunga na Inter Miami zinaonekana kuwa nyingi kutokana na ushawishi mkubwa uliopo wa mmiliki wa timu hiyo, David Beckham ambaye ana uhusiano mzuri na staa huyo.
Hata hivyo, Messi hajaonyesha kiwango bora tangu msimu huu uanze akiwa na PSG akicheza mechi 23 za michuano yote na kufunga mabao saba sambamba na kutoa asisti 11 kwa mabingwa hao wa Ufaransa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Salah wa Liverpool Aingia Rada za PSG na Barcelona​

Mohamed-Salah.jpeg

MOHAMED Salah mshambuliaji wa Liverpool anatajwa kuingia katika rada za PSG na Barcelona ambazo zinahitaji saini yake.
Mkataba wake ndani ya Liverpool kwa sasa una uhai wa miezi 18 na unatarajiwa kumeguka 2023.
Mpaka sasa hakujawa na taarifa yoyote kutoka Liverpool ambao walikaa naye mara ya mwisho Desemva mwaka jana kuhusu kuboresha mkataba wake.
Staa huyo raia wa Misri ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Jurgen Klopp ambage alisistiza kwamba anahitaji huduma ya nyota huyo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Kiungo mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala (28) anatarajia kuondoka klabuni hapo ifikapo mwishoni mwa msimu huu atakapomaliza mkataba wake
Mpaka sasa Dybala hajaonyesha mpango wa kutaka kusalia klabuni hapo
Chanzo: Fabrizio Romano
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nyasi