Ushindi wa Yanga dhidi ya KMC leo ni ishara kwamba Simba wasahau ubingwa?

Feb 7, 2023
61
36
5
Yanga jioni ya leo wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KMC,baada ya ushindi huo ni rasmi sasa yanga watakuwa kileleni kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya mpinzani wake Simba.

Yanga leo wamecheza kibingwa zaidi hawakuhitaji kucheza soka safi sana ila no kutafuta matokeo ya alama tatu.

Kocha Nabi amefanya mabadiliko mengi kwenye kikosi chake leo, ili kupumzisha sehemu kubwa ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao watakuwa na mchezo mgumu dhidi ya Real Bamako ya Mali.

Kwa matokeo ya leo Yanga wanafikisha alama 62 huku mpinzani wake akibakia na alama 54 baada ya kupata sare dhidi ya Azam jana.

Je, kwa msimamo ulivyo unafikiri Simba wanaweza kupambania nafasi ya ubingwa wakati huo Yanga akihitaji kushinda mechi tano kati ya saba zilizobaki kutangaza ubingwa?20230222_180032.jpg