Vipers waibe Notice za Simba CAF

Feb 7, 2023
61
36
5
Wakati Simba wanaingia hatua ya makundi kwa mara ya kwanza walikuwa kundi moja na miamba Al Ahly na As Vita, walipoenda kucheza nao walifungwa magoli matano kwa kila mechi.

Lakini Simba kutokana na ugeni wao kwenye michuano hiyo walianza kujifunza kwamba mechi za ugenini unatakiwa kuchezaje, baada ya hapo iliyobaki ni historia.

walianza kupambania alama kwenye viwanja vya ugenini, hata kama walikosa Lakini kuna uwezo walionyesha kwenye kujilinda zaidi ili kupunguza idadi ya magoli.

Hiki ndio kitu ambacho wanakutana nacho Vipers ya Uganda, jana walifungwa magoli matano dhidi ya Raja Casablanca hii imechangiwa na kukosa nidhamu kwenye eneo Lao la ulinzi walitaka kupishana zaidi na timu iliyokuwa bora zaidi yao.

Naamini sasa watajifunza kutoka kwa Simba kwa kuanza kupambania angalau alama moja ugenini na kuhakikisha unavuna alama tatu nyumbani.

So far Vipers bado timu changa sana kwenye michuano hii ni mara ya kwanza wanaingia hatua ya makundi, so kufika hapa ni hatua kubwa kwao kwa sasa wanahitaji Experience na Exposure ya michuano kwanza kabla hawajaanza kushindana rasmi wakati mwingine.20230211_093625.jpg
 
  • Like
Reactions: jamal and Brenda