Visit Tanzania imeanza kulipa?

Feb 7, 2023
61
36
5
Jezi za Simba wanazozitumia kwenye CAFCL wanatumia Visit Tanzania kama mdhamini wao mkuu kwa sababu mdhamini wao M-bet hawezi kutumika katika hatua ya makundi.

Hii inatokana na mdhamini mkuu wa CAF ni 1xbet hivyo italeta shida kwenye masuala ya kibiashara ( Business Competition).

Kutumika kwa Visit Tanzania kwenye jezi za Simba inaonekana imeanza kulipa baada ya wipanzani wao Raja Casablanca kutumia kivutio kimojawapo cha hifadhi ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ni faida kwa Taifa kwa sababu itasaidia kuleta watalii kutoka mataifa mbalimbali kutoka na FAN BASE kubwa ya Raja Casablanca duniani kote.

Visit Tanzania mbele ya jezi za Simba ni platform kubwa kwa vivutio vyetu hapa nchini, kwa sababu Simba ni chapa kubwa kwa sasa Afrika na duniani kwa ujumla.20230214_095829.jpg