VITA YA MESSI NA RONALDO

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
TIMU ya Manchester United itamenyana na Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Mabingwa watetezi, Chelsea watavaana na timu nyingine ya Ufaransa, Lille.

Katika droo iliyopangwa leo Jijini Nyon nchini Uswisi, timu nyingine za England, Liverpool itamenyana na FC Red Bull Salzburg ya Austria na Manchester City itavaana na Villarreal ya Hispania.

Mechi za kwanza zitachezwa Februari 15, 16, 22 na 23 na marudiano Machi 8,9,15 na 16 mwakani.
Mechi kati ya Manchester United na PSG zinatarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee zikiwakutanisha tena wanasoka wapinzani wakubwa, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Kama unatengeneza mkeka, unampa nani hapo?